Featured Kitaifa

ASKOFU DK. SHOO AFUNGUA MKUTANO WA 86 WA TCMA,ATOA MAAGIZO MATANO KWA TCMA

Written by mzalendoeditor
ASKOFU Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt. Fredrick Shoo,akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 86 wa Chama Cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) ulioanza  leo Septemba 4,2023 Jijini Dodoma.
Na Alex Sonna-DODOMA
ASKOFU Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt. Fredrick Shoo,ametoa maagizo matano  kwa Chama Cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) ikiwemo kujiepusha na vitendo vya rushwa nchini.
Maagizo mengine ni kuzingatia maadili ya Kikristo kwenye utendaji kazi wao,kutoa huduma kwa weledi,ufanisi na ubora wa huduma na kujituma bila kushawishika au kuwa na tamaa ya kujinufaisha.
Dk.Shoo ametoa kauli leo Septemba 4,2023 Jijini Dodoma  wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 86 wa Chama Cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA).
Dk Shoo amesema pamoja na changomoto zote zilizopo Madaktari hao wanatakiwa  kuzingatia maadili ya Kikristo na waendelee kutoa huduma kwa weledi kulingana na taaluma yao.
Pia wazingatie masuala ya ufanisi na ubora wa huduma na kujituma bila kushawishika au kuwa na tamaa yakujinufaisha.
Vilevile amesema  litakuwa jambo jema iwapo watajiepusha na  mienendo inayochafua maadili ya udaktari na kuchafua Kanisa na taaluma ya afya kwa ujumla.
“Muhimu mjiepushe na vitendo vya rushwa na lugha mbaya katika  kuwahudumia wananchi.Kazi ya kuwahudumia wagonjwa ni kazi ya wito  hivyo mnapaswa kufanya kazi kwa moyo wa kuthamini maisha yabinadamu.
“Mmepewa dhamana na mnao wajibu mkubwa wa kutunza heshima ya  taaluma yenu,”amesema Askofu Dkt. Shoo.
Hata hivyo amewahakikishia Madaktari hao wataendelea kuwa nao bega kwa bega katika shughuli zao na kutatua kero mbalimbali.
“Nimefarijika sana kuona Mkutano huu utajadili kikamilifu na kuweka mikakati ya kuweza kuwa makini na ufuatiliaji wa mambo ya msingi na uwajibikaji katika hospitali zetu,”amesema Askofu Dk Shoo.
Amesema   maazimio ya  mkutano huo yatatumika katika kuboresha yale mapungufu yaliyopo kwa pamoja na kuhakikisha huduma za Afya zinazotolewa na Kanisa zinaboreshwa zaidi na kuwa za mfano na endelevu katika jamii.
Aidha ametoa  rai kwa TCMA kwa kushirikiana na CSSC kutengeneza mpango wa utekelezaji wa maazimio ya mkutano huo,”amesema Dk Shoo.
Kwa upande wake Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) ,Dk Paul Kisanga amesema wanatambua  jinsi Serikali inavyothamini mchango wa Kanisa nchini katika kuendeleza jamii kwenye maisha bora.
Aidha amelipongeza kanisa kupitia Taasisi  mwavuli ya CSSC kwa  kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuandaa na kuboresha miongozo ya ushirikiano baina ya Serikali na Watoa huduma za Afya wa Sekta Binafsi (Public Private Partnership) kupitia Wizara zenye dhamana ya Afya na TAMISEMI.
“Tunaishukuru pia serikali kupitia wizara zake hizi mbili kwa kuingia mikataba na baadhi ya hospitali za kanisa katika  ngazi mbalimbali hapa nchini,”amesema Dk Kisanga
Amesema  lengo kuu la ushirikiano huo ni kuboresha huduma za afya katika vituo mbalimbali kwa kutumia miundo mbinu ambayo tayari ilikuwepo ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.
Hata hivyo  amesema  Hospitali na vituo vya kanisa hufanya kazi na serikali kupitia mikataba (Service agreement) na halmashauri husika.
Amesema  pamoja na nia njema ya serikali ya kufanya kazi na taasisi za serikali kwa kupitia mapango wa ‘PPP’, utekelezaji wa mikataba hiyo umekuwa na changamoto kadhaa ikiwemo baadhi ya halmashauri kusita kuendelea  kusaini mikataba inapoisha.
“Na  hata kama vituo husika vinaendelea kutumia rasilimali za Serikali na  kutoa huduma kama awali.Hii inapelekea kuwa na hoja za kiukaguzi kutoka Ofisi ya Taifa ya  Ukaguzi (CAG) zinazaohitaji vituo vya Kanisa kutolea ufafanuzi,”amesema Dk Kisanga
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Christian Social Services Commission (CSSC) Bw.Peter Maduki, amesema tume hiyo imetekeleza maelekezo ya bodi ya kuanzisha mfuko wa uwekezaji wa afya ili kuondokana na kero za kukosa fedha za kulipa mishahara, kununua dawa na vifaa tiba.
“Tumepata mdau kutoka Uingereza ambaye atatupa Sh.Bilioni tisa ili taasisi za afya zikope na kulipa kwa tarakimu moja, hatua hii itawezesha kukopa kulipa mishahara, dawa na vifaa tiba,”amesema Bw.Maduki
Aidha ameeleza  kuwa tayari hospitali 10 zipo kwenye mchakato wa kuthibitisha kama zinaweza kupokea fedha hizo na kuzitumia kiadilifu na kwa ukamilifu.
ASKOFU Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt. Fredrick Shoo,akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 86 wa Chama Cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) ulioanza  leo Septemba 4,2023 Jijini Dodoma.
Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) ,Dk Paul Kisanga,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 86 wa Chama Cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) ulioanza  leo Septemba 4,2023 Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya Hamad Nyemboa,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 86 wa Chama Cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) ulioanza  leo Septemba 4,2023 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka TAMISEMI Dkt.Paul Chaote,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 86 wa Chama Cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) ulioanza  leo Septemba 4,2023 Jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt. Fredrick Shoo (hayupo pichani),wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 86 wa Chama Cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) ulioanza  leo Septemba 4,2023 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Christian Social Services Commission (CSSC) Bw.Peter Maduki,akitoa neno la shukrani mara baada ya Akofu  Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt. Fredrick Shoo,kufungua Mkutano Mkuu wa 86 wa Chama Cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) ulioanza  leo Septemba 4,2023 Jijini Dodoma.
ASKOFU Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt. Fredrick Shoo,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 86 wa Chama Cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) ulioanza  leo Septemba 4,2023 Jijini Dodoma.

About the author

mzalendoeditor