Featured Michezo

SHEREHE ZA UFUNGUZI WA MASHINDANO YA KIHISTORIA YA AFRICAN FOOTBALL LEAGUE (AFL) KUFANYIKA OKTOBA 2023 NA KUFUATIWA NA DROO SIKU YA JUMAMOSI, SEPTEMBA 2.

Written by mzalendoeditor



Klabu bora zaidi barani Afrika zitachuana katika mashindano ya Kihistoria ya African Football League (AFL) yanayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Sherehe ya ufunguzi wa mechi ya kwanza ya mashindano ya AFL itafanyika Jijini Dar es Salaam Oktoba 20 mwaka huu.

Ligi hiyo ya Soka ya Afrika (AFL) imeundwa ili kuonyesha wachezaji bora wa soka wa klabu za Afrika na kuwapa mashabiki wa kandanda barani Afrika na ulimwengu mzima, fursa ya burudani, kwa kuona na kufurahia mchezo bora kabisa katika Bara la Afrika.

Mashindano hayo yataanza kwa hatua ya robo fainali yakifuatiwa na nusu fainali itakayofanyika kati ya tarehe Oktoba 29 na Novemba 1. Fainali zitakazoamua mshindi wa shindano la Uzinduzi wa AFL zitafanyika tarehe 5 na 11 Novemba 2023.

Ratiba ya mashindano ya kwanza ya AFL, ambayo ni ushirikiano kati ya CAF na FIFA imeundwa kwa misingi ya mechi za nyumbani na ugenini na itaanza kwa hatua ya robo fainali ya mtoano.

Mashindano ya AFL yanafanyika kwa ubia kati ya CAF na FIFA. Mashindano hayo yatahusisha timu 8 bora barani Afrika kutoka kanda tatu za Kaskazini, Afrika ya Kati na Magharibi na Ukanda wa Kusini- Mashariki.

Timu za Al Ahly SC, Tunisia’s Esperance de Tunis na Wydad Club Athletic kutoka Morocco ni vilabu vya kandanda kutoka Kanda ya Kaskazini. Miamba wa Soka, Enyimba ya Nigeria na Tout Puissant Mazembe ya DRC ndio Vilabu kutoka Ukanda wa Kati-Magharibi

Mamelodi Sundowns kutoka Afrika ya Kusini, Angola’s Petro Atletico do Luanda na Klabu ya Simba SC kutoka Tanzania ni vilabu kutoka ukanda wa Kusini-Mashariki.

Droo ya uzinduzi wa AFL itafanyika mjini Cairo, Misri septemba 2,2023 na yataruka mubashara kupitia tovuti ya AFL na matangazo ya moja kwa moja kupitia runinga

Ratiba ya mashindano ya kwanza ya AFL, ambayo ni ushirikiano kati ya CAF na FIFA imeundwa kwa misingi ya mechi za nyumbani na ugenini na itaanza kwa hatua ya robo fainali ya mtoano.

Mashindano haya ya kihistoria yatafanyika kwa muda wa wiki nne, yakianza na halfa ya ufunguzi na mechi ya kwanza siku ya tarehe 20 Oktoba 2023 jijini Dar es Salaam.

Nusu fainali itafanyika kati ya Oktoba 29 na Novemba 1. Mechi ya fainali ambayo itaamua mshindi wa AFL itafanyika kati ya Novemba 5 na 11, 2023.

Mashindano ya AFL ni mwanzo wa mashindano makubwa ya Afrika ambayo yatashirikisja timu 24 bora zaidi barani Afrika na yataanza kutimua vumbi katika msimu wa soka wa 2024/2025.

Mashabiki na wapenzi wa soka barani Afrika wanaweza kufuatilia taarifa za mashindano haya kupitia tovuti ya AFL www.afl.africa pamoja na mitandao ya kijamaa kama Facebook, Instagram and X (Twitter).

Fuatilia kupitia tovuti www.afl.africa

Mitandao ya kijamii fuata kurasa;

Facebook: afl_africa

Instagram: afl_africa

X (Twitter): afl_africa</div

About the author

mzalendoeditor