Featured Michezo

YANGA SC YARUDI KILELENI KWA KISHINDO

Written by mzalendoeditor

 

MABINGWA Watetezi Timu ya Wananchi Yanga SC imerudi kileleni Mwa Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara baada ya kuizamisha mabao 5-0 Timu ya JKT Tanzania Mchezo uliochezwa uwanja wa Chamazi Complex Jijini Dar es Salaam.

Yanga SC walienda mapumziko wakiwa mbele ya bao moja lililofungwa na Stephane Aziz Ki kwa Free kick dakika ya 45 +3 baada ya Musonda kuchezewa rafu karibu na lango kla JKT lililoenda moja kwa moja na kumshinda golikipa wa JKT.

Kipindi cha pili kilikuwa kibaya kwa JKT baada ya kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara tatu Yanga SC walipata bao la pili mnamo dakika ya 54 likifungwa na Mshambuliaji Kennedy Musonda akimalizia pasi ya Nickson Kibabage.

Yanga waliendelea kulisakama lango la wapinzani na katika dakika ya 64 beki kitasa kwa sasa kwenye Ligi Kuu Yao Attohoula Kouassi alipiga chuma cha tatu kwa bao safi kwa kuachia shuti kali lililoenda moja kwa moja kwenye Nyavu.

Kipenzi cha wanayanga kijana wa kuchomekea Max Nzengeli alihitimisha safari ya kufunga mabao matano akifunga katika dakika ya 79 na 87.

Kwa ushindi huo Yanga SC wamerudi Kileleni kwa kufikisha Pointi 6 sawa na Azam FC na Simba SC Yanga SC wakiwa na idadi kubwa ya mabao wakifunga mabao 10 na kutoruhusu bao lolote.

About the author

mzalendoeditor