Featured Kitaifa

PROF. KIPANYULA AWASILI NELSON MANDELA TAYARI KUTEKELEZA MAJUKUMU

Written by mzalendoeditor

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia  Professa  Maulilio Kipanyula  akiongea na watumishi wa taasisi hiyo mara baada ya kuwasili

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia  Professa  Maulilio Kipanyula  akisaini  kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika taasisi hiyo

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia  Professa  Maulilio Kipanyula  (katikati)  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi  wa kwanza kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Bw. Sylvester Kazi , wa pili kulia ni Makamu Mkuu wa Taasisi aliyemaliza muda wake Professa Emmanuel Luoga  na wa kwanza Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango,Fedha na Utawala Professa Suzana Augustino na wa pili Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Elimu, Utafiti na Ubunifu Professa Anthony Mshandete.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia  Professa  Maulilio Kipanyula  (katikati aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Taasisi.

Na.Mwandishi Wetu.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia Profesa  Maulilio Kipanyula amewataka Watumishi wa taasisi hiyo, kumpa ushirikiano katika kufikia lengo la kuanzishwa kwa Taasisi hiyo.

Professa Kipanyula ameyasema hayo tarehe 18 Agosti, 2023 alipotembelea  Taasisi ya  Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia  tangu kuteuliwa  kwake na Mkuu wa Taasisi hiyo Bw. Omari Issa mnamo tarehe 14 Agosti ,2023.

“Naomba ushirikiano ,umoja na upendo mliouonesha leo uendelee kati yetu ili kwa pamoja tuweze kuendeleza taasisi hii kwa misingi na malengo ya kuanzishwa kwake” anasema Professa Kipanyula

Profesa Kipanyula ameeleza kuwa katika kutekeleza majukumu ya Taasisi atahakikisha vipaumbele vya Taasisi vinazingatia mipango mikubwa ya Serikali  hususani Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Vilevile Professa Kipanyula alipata wasaa wa kukabidhiwa ofisi na Makamu Mkuu wa Taasisi aliyemaliza muda wake Professa Emmanuel Luoga kwa kukabidhiwa vitendea kazi ambavyo ni dira na muongozo wa utekelezaji wa majukumu yake.

“Natambua kazi nzuri iliyofanywa na mtangulizi wangu Professa Emmanuel Luoga, kwa uongozi mahiri alioufanya na kufanikisha kukifikisha chuo mahali pazuri” Amesema Profesa Kipanyula

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Bw. Sylvester Kazi amempongeza  Professa Kipanyula kwa uteuzi wake na kumuahidi kuendeleza ushirikiano kama ambavyo walikuwa wakishirikiana awali katika baraza la chuo.

About the author

mzalendoeditor