Featured Kitaifa

VIJANA WAPONGEZWA KWA KUCHANGAMKIA FURSA YA BBT

Written by mzalendoeditor

 

Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Leonard Mchau akizungumza na Vijana katika Kituo cha Mafunzo ya Wakulima na Kuhimilisha Vijana Bihawana  Jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Leonard Mchau (wa pili kutoka kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi Ally Msaki (wa pili kutoka kulia) walipotembelea Kituo atamizi cha Vijana mradi wa BBT Jijini Dodoma, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo Robert Masingiri.

Na. Mwandishi wetu, Dodoma.

Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu imewapongeza vijana kwa kuchangamkia fursa ya programu ya Taifa ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) inayoratibiwa na Wizara ya Kilimo kwa Kushirikiana na Ofisi hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa Agosti 18, 2023 na Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Leonard Mchau alipotembelea Kituo cha mafunzo ya wakulima na kuhimilisha vijana cha Bihawana na Chinangali mkoani Dodoma.

Amesema licha ya baadhi ya vijana hao kuwa na elimu ya juu lakini wameamua kujikita katika kilimo ili kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wao, Wanufaika wa Programu hiyo, Aseiblem Msuya na Baraka Issa , wameishukuru serikali kwa kuwapa mafunzo hayo ya kilimo na kuwahimiza vijana kutumia fursa zinazotolewa na serikali ikiwamo BBT ili kujikwamua kiuchumi.

About the author

mzalendoeditor