Featured Kitaifa

WAZIRI MKENDA ATETA  NA MKURUGENZI MKAZI WA BENKI YA DUNIA NCHINI TANZANIA

Written by mzalendoeditor

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Julai 17, 2023 jijini Dar es Salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Nchini Tanzania Bw. Nathan Belete na ujumbe wake.

Kikao hicho kilikuwa na lengo la kujadili mpango pendekezwa wa utekelezaji wa mageuzi ya Elimu na ushirikiano na Benki ya Dunia katika
utekelezaji huo.

Aidha wamekubaliana kuboresha miradi ya BOOST na SEQUIP ili iweze kukidhi kuwezesha mahitaji ya utoaji elimu ujuzi pamoja na kujadili maendeleo ya Miradi mingine katika ngazi ya elimu ya ufundi.

     

About the author

mzalendoeditor