Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan apokea Taarifa ya Tume ya Kuangalia Jinsi na Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai hapa Tanzania kutoka kwa Jaji Mstaafu Mh. Mohammed Chande Ikulu Jijini Dar es Salaam Leo Julia 15, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassanakizungumza mara baada ya kupokea Taarifa ya Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai hapa Tanzania, Ikulu Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Tume ya Kuangalia Jinsi na Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai hapa Tanzania kutoka kwa Jaji Mstaafu Mh. Mohammed Chande akizungumza wakati wa kukabidhi taarifa hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Kuangalia Jinsi na Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai hapa Tanzania kutoka kwa Jaji Mstaafu Mh. Mohammed Chande akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wenzake wakati wa kukabidhi taarifa hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Leo.
Kutoka Julia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Mpogole Kusiluka na Katibu Mkuu Kiongozi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassana,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea Taarifa ya Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai hapa Tanzania, Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amezitaka taasisi za haki jinai kufanya marekebisho ambayo hayana gharama za kifedha katika mifumo yao ya kiutendaji ili kuleta haki kwa wananchi.
Rais Samia ameyasema hayo leo wakati akipokea taarifa rasmi ya Tume ya Kuangalia jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai hapa nchini katika hafla iliyofanyika Ikulu.
Aidha, Rais Samia amesema ni vyema marekebisho hayo yafanyike kabla ya mabadiliko ya kiutawala na kiufundi yanayoigharimu serikali fedha nyingi.
Rais Samia pia ameelekeza kufanyiwe kazi masuala ya kuheshimu watuhumiwa kwenye ukamataji, upelelezi pamoja na uendeshaji wa mashtaka mbalimbali ili haki iweze kutendeka.
Vile vile, Rais Samia amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama visitoe kipaumbele katika kukamata na kuhukumu na badala yake vijikite kuzuia kutenda makosa.
Kwa upande mwingine Rais Samia amevitaka vyombo vya jinai kuwa na mfumo unaosomana katika uendeshaji ili kurahisisha ufuatiliaji pamoja na kuzuia mfumo wa upelelezi kutoa mwanya wa rushwa.
Tume ya Haki Jinai iliyoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman ilikusanya maoni kutoka taasisi 12 kwa lengo la kupata ushauri na mapendekezo ya namna bora ya kuimarisha mfumo na utendaji kazi wa taasisi zinazohusika na haki jinai.