Mkurugenzi wa huduma za Mawasiliano, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mulembwa Munaku ,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kufungwa kwa program ya zungumza na Dkt. Samia ambayo ina lengo la kutoa Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanachama wa wanawake na Uchumi wa viwanda (WAUVI) leo Mei 30,2023 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa kilimo na Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde,akipata maelezo kwa Mtaalum wa mfumo wa Anwani za Makazi Bw.Innocent Jacob kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari kwenye banda la Wizara hiyo wakati wa Maonyesho ya Program ya zungumza na Dkt. Samia ambayo ina lengo la kutoa Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanachama wa wanawake na Uchumi wa viwanda (WAUVI) leo Mei 30,2023 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa kilimo na Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde,akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Kitaifa wa Mfumo wa Anwani za Makazi kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari kwenye banda la Wizara hiyo wakati wa Maonyesho ya Program ya zungumza na Dkt. Samia ambayo ina lengo la kutoa Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanachama wa wanawake na Uchumi wa viwanda (WAUVI) leo Mei 30,2023 jijini Dodoma.
Na Dotto Kwilasa, DODOMA.
Mkurugenzi wa huduma za Mawasiliano, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mulembwa Munaku amewataka wananchi kuheshimu miundombinu ya mfumo wa anwani za makazi ili kurahisisha huduma za kijamii na kuchochea uchumi.
Bw.Munaku amesema hayo leo Mei 30,2023 Jijini Dodoma kwenye mafunzo ya wajasiriamali kwa wanachama wa wanawake na uchumi na kuongeza kuwa suala la taarifa za anwani za makazi linakuwa la msingi wakati wa kutoa na kupokea huduma bidhaa kwa kujumuisha mifumo ya kielekroniki.
Akizungumza kwenye mafunzo hayo ambayo pia yamejumuisha namna mfumo wa kidigitali wa anwani za makazi (NaPA)unavyofanya kazi, Bw.Munaku amesema huwezi kutofautisha
suala la amwani za makazi na wafanyabiasha kwa kuwa maendeleo ya biashara yanatokana na biashara mtandao.
“Jumla ya anuani milioni 12 zimesajiliwa nchi nzima,kupitia simu ya mkononi mwananchi anaweza kutambua anuani yake ya makazi,hata hivyo bado kuna changamoto zilizopo za uharibifu wa miundombinu wa makusudi nitoe wito acheni tabia hiyo,”amesisitiza na kuongeza;
Kila mtu anawajibika kulinda alama zote za mfumo huu, makazi ya watu yanapewa namba ili kutambulika na kufikiwa kwa urahisi Sasa unapoharibu Kwa makusudi unakwamisha maendeleo ya watu Kwa kuwa sehemu zao hazitatambulika,”Anasema.
Pamoja na hayo Munaku amezitaja faida za mfumo wa anuani za makazi kuwa ni pamoja na kurahisisha kufikiwa kwa maeneo mengi kwa ajili ya huduma mbalimbali ikiwemo biashara na
kuwezesha kupanga na kusimamia mipango mahsusi ya kutoa huduma kwa wananchi.
Munaku amesema miundombinu hiyo ikitunzwa na kuheshimiwa itarahisisha utoaji wa huduma za dharura kama vile uokoaji na kukabiliana na maafa ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa makazi ya watu.
“Tupo hapa Kwa ajili ya kuwaelimisha wafanyabiashara umuhimu wa anuani za makazi,wanatakiwa kujua ni muhimu kujisajili na kuraaimisha makazi yao ili kurahisisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi kwa makusudi mbali mbali,”amesema
Amefafanua kuwa miundombinu ya anuani za makazi pia inasaidia kuimarisha utawala bora na kuigusa jamii moja Kwa Moja katika afya,elimu na biashara.