Featured Kitaifa

SERIKALI YASAINI MKATABA DMDP AWAMU YA PILI JIJINI DODOMA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angellah J. Kairuki akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu L. Nchemba pamoja na viongozi wengine wakishuhudia utiaji saini wa mkataba wa mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP 2) katika Manispaa za Kinondoni na Ubungo chini ya Mhandisi Nimeta Consult (t) Ltd katika hafla hiyo fupi iliyofanyika leo Mei 30,2023  jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu L. Nchemba pamoja na viongozi wengine wakishuhudia utiaji saini wa mkataba wa mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP 2) katika Manispaa za Temeke na Kigamboni chini ya Mhandisi Consultancy Ltd & Luptan katika hafla hiyo fupi iliyofanyika leo Mei 30,2023 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angellah J. Kairuki akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu L. Nchemba pamoja na viongozi wengine wakishuhudia utiaji saini wa mkataba wa mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP 2) katika Manispaa za Kinondoni na Ubungo chini ya Mhandisi Nimeta Consult (t) Ltd katika hafla hiyo fupi iliyofanyika leo Mei 30,2023  jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angellah  Kairuki akizungumza na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP 2) iliyofanyika leo Mei 30,2023  jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki akizungumza na viongozi wa Wizara, Wabunge pamoja na Wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP 2) iliyofanyika leo Mei 30,2023 jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu L. Nchemba  akizungumza na viongozi wa Wizara, Wabunge pamoja na Wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP 2) iliyofanyika leo Mei 30,2023 jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa na Mbunge wa Mikumi Mhe. Dennis Londo akitoa salamu za Kamati hiyo katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP 2) iliyofanyika leo Mei 30,2023  jijini Dodoma.

 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango  Dkt. Natu El -Maamry,akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba ya mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP 2) iliyofanyika leo Mei 30,2023  jijini Dodoma.

Mratibu wa Mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam (DMDP), Mhandisi Humphrey Kanyenye akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP 2) katika hafla hiyo fupi iliyofanyika leo Mei 30,2023 ukumbi wa Mkapa jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Dar es salaam na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dkt. Faustine Ndugulile akitoa salamu za Wabunge wa Majimbo ya Mkoa wa Dar es salaam katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya mradi wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP 2) iliyofanyika leo Mei 30,2023  jijini Dodoma.

  Na.Alex Sonna-DODOMA

SERIKALI  imeingia mkataba wa Makubaliano ya Mradi Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam(DMDP) awamu ya pili na wakandarasi watatu wenye thamani ya shilingi Bilioni 800 huku ikiahidi kusimamia mradi huo ili ukamilike kikamilifu.

Akizungumza leo Mei 30,2023  jijini Dodoma mara baada ya kushuhudia utiaji saini kati ya TAMISEIMI na wakandarasi watatu watakaosanifu mradi huo katika halmashauri tano za Mkoa wa Dar es Salaam,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Angellah Kairuki, amesema ofisi yake itahakikisha utekelezaji huo unakuwa na mafanikio makubwa

Mhe.Kairuki amesema kuwa mradi huo unakwenda kutatua kero mbalimbali ikiwamo ujenzi holela wa makazi, miundombinu duni ya usafiri, mabadiliko ya tabia nchi kwa jiji la Dar es Salaam zinazosababisha mafuriko na utupaji taka ngumu ovyo.

“Wabunge wa maeneo husika hakikisheni mnasimamia halmashauri zenu ili utekelezaji wa mradi huu uwe na mafanikio na kusiwepo dosari, TAMISEMI tutakuwa makini kuhakikisha kwamba mradi huu awamu ya pili unatekelelezwa kwa mafanikio makubwa, tunaamini tutakuwa tumejifunza kupitia utekelezaji wa awamu ya kwanza,”amesema 

Hata hivyo amewataka  makandarasi ambao watatekeleza mradi huo kutoka Mhandisi Consultancy LTD & Luphan(Halmashauri ya Temeke na Kigamboni), Nimeta Consultancy LTD(Halmashauri ya Kinondoni na Ubungo) na UWP Consultancy LTD(Halmashauri ya Dar es Salaam) kuzingatia masharti ya mikataba yao.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta Mwigulu Nchemba amesema ujio wa mradi huo umeleta faraja kwa wabunge wa Dar es salaam ambao wamekuwa wakiuzungumzia mara kwa mara.

Akitoa taarifa ya mradi, Mratibu wa miradi ya Serikali kupitia mikopo ya Benki ya Dunia, Tamisemi na Tarura, Mhandisi Humphrey Kanyenye amesema jiji la Dar es Salaam lina changamoto ya usanifu, utunzaji taka ngumu, mafuriko na miundombinu isiyokidhi hivyo mradi huo unaenda kuziondoa.

“Asilimia 74 ya fedha hizi zitatumika kwenye miundombinu kukarabati barabara, mifereji, maeneo ya wazi, masoko, vituo vya mabasi, kurekebisha miundombinu ya taka ngumu na utekelezaji unatarajiwa kuanza Aprili 2024,”amesema Mhandisi Kanyenye

Naye Mwenyekiti wa wabunge wa Mkoa huo, Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile ameishukuru serikali kwa utekelezaji wa mradi huo na kutoa angalizo kwamba wao kama wawakilishi wa wananchi watasimama kidete kuhakikisha unafanikiwa.

Dk.Ndugulile  amesema kwa Mkoa wa Dar Es Salaam Kipaumbele cha kwanza ni barabara cha pili barabara na cha tatu ni barabara na kufafanua kuwa hali hiyo inadhihirisha wazi kuwa wananchi wanahitaji barabara kabla ya mambo mengine.

Amesema Mkoa huo unapaswa kupewa kipaumbele hasa Kutokana na mchango wake kwenye masuala ya uchumi wa nchi.

“Lazima tuupe kipaumbele Mkoa huu,barabara zake hazilingani na mchango wake kwenye uchumi,tunataka Jiji la hili liwe na muundo na uendeshaji tofauti na mikoa mingine, tunatambua barabara ni maisha , barabara ni uchumi,”amesema

Utekelezaji wa mradi huo utaanza April mwaka 2024 ambapo asilimia 74 ya fedha zitatumika kukarabati barabara, mifereji, maeneo ya wazi, masoko, vituo vya mabasi, kurekebisha miundombinu ya taka ngumu, kujenga uwezo kwa halmashauri hizo.

About the author

mzalendoeditor