Featured Kitaifa

HEDHI SALAMA BADO CHANGAMOTO SHULENI

Written by mzalendoeditor
NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO.
Shule za msingi na sekondari za Mkoa wa Morogoro zinakabiliwa na ukosefu wa miundombinu wezeshi kwa wanafunzi wa kike wenye umri wa kuingia hedhi ikiwemo ukosefu wa vyumba maalumu ya kubadilishia taulo, maji safi pamoja na tanuru za kuchomea taulo zilizotumika hali inayosababisha baadhi ya wanafunzi hao kushindwa kuhudhuria masomo wanapokuwa hedhi.
Hayo yameelezwa kwenye maadhimisho ya siku ya hedhi duniani yalioandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Chalice na kufanyika Shule ya Sekondari ya Nelsonimandera ambapo wanafunzi wa shule hiyo wamesema wanapata wakati mgumu wanaingilia kwenye hedhi jambo linaloasili maudhulio yao ya shule na kushindwa kufanya vizuri katika masomo.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Mratibu wa programu ya CHALICE Halifa Khan aamesema wapo tayari kushirikiana na serikali katika kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanapata hedhi salama ili waweze kutimiza ndoto zao.
Amesema Katika kuhakikisha mabinti wote wanapata haki ya kupata Hedhi Salama shirika Kwa kushirikiana na Serikali, kupitia mradi wa LESAPA wanatengeneza taulo za kike na kuzigawa kwenye shule za msingi na Sekondari ili kuondoa changamoto wanazokutanazo na kushindwa kuhudhulia masomo.
“Leo tumegawa taulo za kike za kufua kwa shule za sekondari na msingi ambazo mabinti wanaweza kuzitumia mwaka mmoja pamoja na kuwapa elimu mabinti juu ya hedhi salama.”alisema bwana Khan.
Nae Mwenyekiti kituo cha tarifa na maarifa (TGNP) kutoka Kata ya Mkabarani Theresia Beregi ameiomba serikali kuweka bejeti ya taulo za kike katika shule za msingi kwani mabinti wengi wamekuwa wakianza kupata hedhi wakiwa na umri mdogo.
“Hapo awali mabinti walikuwa wanapata hedhi wakiwa na miaka kumi na mbili mpaka kumi na sita lakini siku hizi ni tofauti mtoto wa miaka tisa mpaka kumi anapata hedhi kimsingi huyo bado yupo shule ya msingi.”alisema Bi Theresia

About the author

mzalendoeditor