Featured Michezo

HISTORIA YAANDIKWA YANGA SC YATINGA FAINALI CAF CONFEDERATION

Written by mzalendoeditor

Na.Alex Sonna

Histori imeandikwa Tanzania,Afrika Mashariki na Kati Timu ya Yanga SC imetinga Fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuwazamisha mabao 2-1 wenye  Marumo Gallants mchezo uliopigwa uwanja wa Royal Bafokeng jijini Rustenburg nchini Afrika Kusini.

Wakicheza kwa nidhamu na kwa utulivu huku wakishambulia kwa kushtukiza Yanga SC walipata bao la kwanza dakika ya 45 likifungwa na Mshambuliaji hatari kwa sasa  Fiston Mayele baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Marumo.

Kipindi cha pili wenyeji walianza mpira kwa kasi hata hivyo mashambulizi yao hayakuzaa bao na katika dakika ya 63 Kennedy Musonda alipigilia msumari wa pili akimalizia pasi ya Fiston Mayele.

Wenyeji walipata bao la kufutia machozi limefungwa na Mshambuliaji wao hatari Ranga Chivaviro ambaye amefikisha mabao 6 sawa na Mayele.

Kwa ushindi huo Yanga SC wameandika historia ya kutinga Fainali ya CAF na sasa wanasubiri mshindi kati ya USM Alger dhidi ya ASEC Mimosas watakaocheza majira saa nne usiku Fainali ya kwanza itachezwa Mei 28 na mechi ya marudiano itachezwa Juni 3,mwaka huu.

About the author

mzalendoeditor