Featured Kitaifa

WADAU WAKUTANA KUFANYA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MPANGO KAZI WA KITAIFA WA KUZUIA BIASHARA HARAMU YA KUSAFIRISHA BINADAMU

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Bw.Kaspar Mmuya,akisisitiza jambo kwa washiriki  wakati akifungua  kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji  wa Binadamu kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Bw.Kaspar Mmuya, akizungumza wakati akifungua  kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji  wa Binadamu kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM)-Tanzania Bw.Maurizio, akizungumza wakati wa  kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji  wa Binadamu kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la UNICEF Joseph Matumbwi ,akizungumza wakati wa  kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji  wa Binadamu kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii Zanzibar Bw.Hassan Ibrahim Suleiman, akizungumza wakati wa  kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji  wa Binadamu kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

Katibu wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu,Seperatus Fella,akizungumza wakati wa  kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji  wa Binadamu kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

  

Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Bw.Kaspar Mmuya (hayupo pichani) wakati akifungua  kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji  wa Binadamu kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Bw.Kaspar Mmuya, akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua   kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji  wa Binadamu kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.

 Alex Sonna-DODOMA

SERIKALI imewataka wadau na  jamii kupaza  sauti kuhusiana na biashara haramu ya kusafirisha binadamu ili Serikali iweze kujua na kuchukua hatua kali kwa wahusika.

Hayo yameelezwa leo Mei 4,2023 jijini Dodoma  na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Bw. Kaspar Mmuya, wakati akifungua  kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa mpango kazi wa kitaifa wa kuzuia na kupambana na biashara haramu ya usafirishaji  wa binadamu.

Bw.Mmuya amesema Wizara yake  inasimamia utekelezaji wa sheria na  kila raia anapaswa azifuate  ikiwa  ni pamoja na kuacha biashara haramu ya kusafirisha binadamu.

“Sasa hivi kuna changamoto  kubwa ya kuiga tabia, tunawachukua watu kwa upendo kumbe tunaenda kuwapeleka katika matendo ambayo sio sahihi ,hapana sio ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”amesema Bw.Mmuya

Bw.Mmuya amesema jamii inapaswa kupaza sauti kuhusiana na jambo hilo ili serikali iweze kujua na kuchukua hatua.

Amesema watunga sera na sheria   ndio wasemaji wazuri wanaotetea  katika ngazi ya jamii ambapo tatizo hilo lipo.

“Wale wakisimama na kulikemea kuwa hili ni tatizo tunaweza kwenda hatua nyingine,unakuta  sisi wenyewe tunasema wale ambao wana platform kubwa ya kusema katika jamii hawana uelewa wa kutosha ama la,”amesema Bw.Mmuya

Hata hivyo Bw.Mmuya amesema wadau hao  katika majukumu yao ni lazima  waelekeze ni kazi zipi zimefanyika kwa ajili ya kuwasaidia wahanga na zimefanyika kwa kiwango  gani na Je malengo yamefikiwa kwa kiwango  gani.

Pia amesema  mikakati au kazi zilizofanywa ili kuimarisha utaratibu na ushirikiano zimefanyika kwa kiasi gani ili wengine wajifunze.

“Msisite kueleza changamoto zipi zimejitokeza katia utekelezaji wa mpango kazi ni muhimu ila hakikisheni mnatofautisha changamoto na udhaifu,madhaifu siku zote ni malalamiko lalamiko tu”amesema Bw.Mmuya

Pia amesema kikao hicho kivumbie na kubainisha fursa zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar.

“Niwaombe mtekeleze kazi ambazo hazijatekelezwa. Thamani ya kazi yenu kwanza ni kujikubali wewe mwenyewe kazi yako inahusiana na utu na matendo ya huruma,”amesema

Kwa upande wake Katibu wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu,Seperatus Fella, amesema lengo la kikao hicho ni  kupitia na kutathmini utekelezaji wa ikiwa ni pamoja na kufanya ufatiliaji ili kuona mafanikio, changamoto zilizokwamisha utekelezaji na kuweka mkakati na mpango kazi madhubuti ili kuboresha utendaji kazi.

Naye Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Zanzibar Bw.Hassan Ibrahim Suleiman, amesema kuwa Idara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Shirika la IOM na Mashirika mengine wamekuwa wakitoa elimu kwa jamii kwa njia mbalimbali, kuwazuia katika maeneo ya Bandari kwa kupata taarifa za matukio hayo na kuwaweka katika nyumba salama kwa malazi, mavazi kuwapatia ujuzi na baadaye kuwarejesha kwao.

Awali Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la UNICEF Joseph Matumbwi , amesema kuwa Usafirishaji Haramu wa Binadamu ni jambo ambalo linawaathiri sana Watoto, hivyo  katika utekelezaji wa mpango kazi  ni vyema kuangalia yale ambayo yanawafaa katika kuhakikisha matamanio yao yanafikiwa, kuwasaidia wahanga kwa kadri ya Sheria inavyotaka, kuwafikisha katika maeneo salama na kuwarudisha katika maeneo wanapotoka.

”UNICEF itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania, Shirika la IOM kwa kufanya kazi na kuweza kuwasaidia Watoto wa Tanzania dhidi ya janga hili hata baada ya kukamilika kwa muda wa mpango.”amesema
 

About the author

mzalendoeditor