Featured Kitaifa

KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA MIAKA 101 YA MWALIMU NYERERE KUFANYIKA DODOMA

Written by mzalendoeditor
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Bw.Peter Mavunde,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Mei 4,2023 jijini Dodoma  kuelekea katika kongamano la kumbukizi ya miaka 101 ya kuzaliwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Na. Gideon Gregory-DODOMA
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la kumbukizi ya miaka 101 ya kuzaliwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Hayo yamesemwa leo Mei 4,2023 jijini Dodoma na Makamu mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Bw.Peter Mavunde wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea katika kongamano hilo.
Bw.Mavunde amesema kuwa   lengo la kuandaa kongamano hilo ni kuwarithisha vijana kuhusu yale yote ambayo Hayati Mwl Nyerere aliyafanya kwa taifa la Tanzania.
“Taasisi iliona mwaka huu iwahusishe vijana wetu, wanafunzi wetu wa vyuo vikuu, vya kati,  shule za msingi na sekondari ili taasisi iwenze kuianza safari ya kuwarithisha vijana wetu wafuate nyendo za mwalimu Julius Kambarage Nyerere mambo mazuri aliyoliyoachia taifa hili, kama mtakumbuka baba wa taifa aliacha alama katika taifa lake, amani lakini Muungano unazidi kuimarika,”amesema Bw.Mavunde
Amesema kuwa Kongamano hilo litafanyika Mei 6,mwaka huu katika Ukumbi wa Chimwanga katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Aidha ameongeza kuwa Mwalimu Nyerere katika farsafa yake kubwa ya ujamaa na kujitegemea ililifanya Taifa la Tanzania na watu wake kuwa na moyo wa kujitegemea hivyo wanahitaji moyo huo kuurudisha kwa vijana.
“Kupitia Kongamano hili pia tutafungua klabu za Mwalimu Nyerere za mazingira katika vyuo vyote na shule zote za msingi na sekondari,”ameongeza.

About the author

mzalendoeditor