MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 2.5 katika eneo la Buigiri, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo Aprili 25,2023
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule,akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph,akitoa taarifa fupi ya mradi wa ujenzi wa tangi lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 2.5 katika eneo la Buigiri, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo Aprili 25,2023
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule,akipokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph,mara baada ya kutoa taarifa fupi ya mradi wa ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 2.5 katika eneo la Buigiri, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo Aprili 25,2023
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 2.5 katika eneo la Buigiri, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo Aprili 25,2023
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule,akizindua mradi wa ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 2.5 katika eneo la Buigiri, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo Aprili 25,2023 .
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule,akifungulia maji mara baada ya kuzindua mradi wa ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 2.5 katika eneo la Buigiri, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo Aprili 25,2023 .
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule,akimtwisha maji Mama mara baada ya kuzindua mradi wa ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 2.5 katika eneo la Buigiri, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo Aprili 25,2023 .
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule,akizungumza na wananchi wa Buigiri mara baada ya kuzindua mradi wa ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 2.5 katika eneo la Buigiri, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo Aprili 25,2023 .
BAADHI ya Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule (hayupo pichani) mara baada ya kuzindua mradi wa ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 2.5 katika eneo la Buigiri, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo Aprili 25,2023 .
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 2.5 katika eneo la Buigiri, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo Aprili 25,2023 .
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Isaya Msuya ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 2.5 katika eneo la Buigiri, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo Aprili 25,2023 .
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 2.5 katika eneo la Buigiri, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo Aprili 25,2023 .
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua mradi wa ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 2.5 katika eneo la Buigiri, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo Aprili 25,2023 .
Na.Alex Sonna-CHAMWINO
MAMLAKA ya Maji safi na usafi wa mazingira Dodoma (DUWASA) imekamilisha mradi wa ujenzi wa tangi lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 2.5 katika eneo la Buigiri, Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Uzinduzi huo umezinduliwa leo Aprili 25,2023 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule,katika Kata ya Buigiri ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba,amesema kuwa wizara yake inaendelea na utekelezaji wa majuumu yake kwa mujibu wa katiba ya nchi, sheria,sera, miongozo pamoja na Ilani ya uchaguzi.
Mhandisi Kemikimba amesema kuwa mahitaji ya maji kwa siku katika jiji la Dodoma ni lita milioni 133.4 na uzalishaji ni lita milioni 67.8 kwa siku upungufu ni asilimia 54 na ongezeko la mahitaji linakuwa kila mwaka.
“Ili kukabili hali hii Duwasa wanaendeleza jitihada za kuboresha huduma za maji ikiwemo kuchimba visima katika eneo la Nzuguni vitakavyo hudumia eneo la Nzunguni,Swaswa na Ilazo”amesema Mhandisi Kemikimba
Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi , amesema lengo la kuadhimisha miaka 59 ya muungano kwa kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo ni kuurudisha kwa wananchi.
“Zamani tulikuwa tuadhimisha Muungano kwa kufanya sherehe za kitaifa lakini kitu ambacho tunakifanya leo ni kuurudisha Muungano kwa wananchi ambao ndiyo wamiliki”amesema Bw.Mitawi
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph,akitoa taarifa fupi ya mradi huo amesema kuwa ujenzi wa tangi hilo umegharimu kiasi cha Sh.bilioni 1.12.
Amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuondoa tatizo la maji katika wilaya ya Chamwino eneo ambalo ipo Ikulu ya Rais.
Hata hivyo amesema kuwa mahitaji ya maji katika eneo hilo ni lita milioni 3.6 na uwezo wa kuzalisha maji kwa siku hivi sasa ni lita milioni 4.4 kwa siku hali inayofanya eneo hilo kuwa na ziada ya maji kwa zaidi ya miaka 30 ijayo.
“Kukamilika kwa mradi huu kumefanya asilimia 87 ya watu wa wilaya ya Chamwino kuwa na uhakika wa maji na umeongeza upatinaji wa maji kwa asilimia 55”amesema Mhandisi Joseph
Aidha amesema kuwa mradi huo ulikuwa umetengewa kiasi cha Sh. bilioni 2.5 lakini kutokana na kutumia mfumo wa Force Account kimetumika kiasi cha Sh. bilioni 1.12 na kuokoa asilimia 50 ya fedha hizo.