RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwanafunzi Hunaina Hamad wa Darasa la Saba wa Skuli ya Msingi ya Kidongochekundu , alionesha jinsi ya uungaji wa umeme wakati alipotembelea Maabara ya Sayansi ya Skuli hiyo baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Skuli hiyo uliofanyika leo 24-4-2023, na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Kitwana Mustaf.(
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwanafunzi wa Darasa la Saba Habal Haji Majid wa Skuli ya Msingi ya Kidongochekundu , alitowa maelezo jinsi ya kujifunnza kupitia Tehama alipotembelea chumba cha Komputa cha Skuli hiyo baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi uliofanyika leo 24-4-2023 na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwapongeza Wanafunzi wa Darasa la Saba wa Skuli ya Msingi ya Kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja wakati akitembelea moja la darasa katika Skuli hiyo baada ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Skuli hiyo, iliyojengwa kupitia fedha za Uviko-19 na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Kitwana Mustafa na (kushoto kwa Rais) Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Ali Abdulgulam Hussein., ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika nac Zanzibar
VIONGOZI wa Serikali, Wabunge, Wawakilishi na Viongozi vya Vyama vya Siasa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Kidongochekundu iliyojengwa kwa fedha za Uviko-19, ikiwa ni shamrashamra za Kuadhimisha Miaka 59 ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika,
WALIMU na Wananchi mbalimbali wakifuatilia hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Jengo jipya la Skuli ya Msingi Kidongochekundi Wilaya ya Mjini Unguja wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwahutubia katika viwanja vya Skuli hiyo baada ya kuweka Jiwe la Msingi la ufunguzi uliofanyika leo 24-4-2023.(Picha na Ikulu)