Featured Kitaifa

RAIS ALHAJJ DK.MWINYI AJUMUIA NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM KATIKA IBADA YA SALA YA EID EL FITRY MASJID JAMIU ZINJIBAR MAZIZINI UNGUJA

Written by mzalendoeditor

 

SHEIKH Ally Abdulrahaman Al Hilaal kutoka Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, akisoma hutuba ya Sala ya Eid El Fitry iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar iliyofanyika leo 22-4-2023, baada ya Waumini wa Dini ya Kiislam kumaliza Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki kuitikia dua ikisoma na Hatibu Sheikh.Ally Abdurahaman Al Hilaal,(hayupo pichani) baada kwa Hutuba ya Sala ya Eid El Fitry iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 22-4-2023, na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Khalid Ali Mfaume na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba, Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.Alhajj Othman Masoud Othman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

BAADHI ya Mabalozi Wagodo wanaofanyia Kazi zao Zanzibar,Viongozi wa Dini na Wananchi wakishiriki katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi,(hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid El Fitry iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki kuitikia dua ikisoma na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Othman Hassan Ngwali (hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid El Fitry iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 22-4-2023, na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba, Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.Alhajj Othman Masoud Othman.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki kuitikia dua ikisoma na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Hassan Othman Ngwali (hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid El Fitry iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 22-4-2023, na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Khalid Ali Mfaume na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba, Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.Alhajj Othman Masoud Othman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

KADHI Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Othman Hassan Ngwali akisoma dua baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid El Fitry iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar iliyofanyika leo 22-4-2023.(kushoto kwake) Viongozi wa Dini na Mabalozi Wadogo Wanaifanyia Kazi zao Zanzibar wakishiriki kuitikia dua.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhajj Dkt. Amani Abeid Karume, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Eid El Fitry, iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 22-4-2023, baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman baada ya sala ya Idd el Fitri  iliyoswaliwa leo katika Masjid Jamighu Zinjibar Mkoa wa Mjini Magharibi(katikati)Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla .

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, baada ya sala ya Idd el Fitri  iliyoswaliwa leo katika Masjid Jamighu Zinjibar Mkoa wa Mjini Magharibi(katikati) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (katikati) baada ya sala ya Idd el Fitri  iliyoswaliwa leo katika Masjid Jamighu Zinjibar Mkoa wa Mjini Magharibi(kulia)Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mussa Mahmoud Wadi.

Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Viongozi mbali mbali wakiitikia Dua baada  kumalizika kwa ibada ya sala ya Idd el Hajj iliyoswaliwa katika Masjid Jamighu Zinjibar Mkoa wa Mjini Magharibi

Waumini wa Dini ya Kiislamu wakisikiliza Khutba ya swala ya Idd -el Fitry iliyotolewa na Sheikh Ali Abdulrahman Al- Hilaal kutoka Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar katika   Masjid Zinjibar Mkoa wa Mjini Magharibi 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Balozi Mdogo wa Oman Aliyepo Zanzibar Mhe.Said Salim Sinawiy  baada ya sala ya Idd el Fitri  iliyoswaliwa leo katika Masjid Jamighu Zinjibar Mkoa wa Mjini Magharibi .

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiwapungia mkono waumini wa dini ya Kiislamu wakati akiondoka katika Masjid Jamighu Zinjibar Mkoa wa Mjini Magharibi  baada ya sala ya Idd el Fitri  iliyoswaliwa leo (kushoto)Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa (kulia).

Baadhi ya watoto waliofika Ikulu Jijini Zanzibar wakisubiri Kupokea Mkono wa Idd  kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi, katika kusherehekea Sikukuu ya Idd el Fitri iliyoanza leo kitaifa

Mkurugenzi Huduma za Rais wa Zanzibar (Mnikulu) Ndg.Mahmoud Othman (kuchoto) akitoa Mkono wa Iddi kwa Watoto waliofika Viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi,katika kusherehekea Sikukuu ya Idd el Fitri iliyoanza leo Kitaifa.

Mhudumu Ofisi ya Rais wa Zanzibar  Ndg.Mohamed Nyahiga(kushoto)  akitoa Mkono wa Iddi kwa Watoto waliofika Viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi,katika kusherehekea Sikukuu ya Idd el Fitri iliyoanza leo Kitaifa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa  akitoa hutuba yake katika Baraza la Eid El Fitri leo lililofanyika katika Ukumbi wa Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, katika kusherehekea Sikukuu ya Idd baada ya kumalizika kwa Mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

[Picha na Ikulu]

About the author

mzalendoeditor