Featured Michezo

BALEKE AING’ARISHA SIMBA SC IKIIKANDA WYDAD CASABLANCA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Written by mzalendoeditor

WAWAKILISHI Pekee  Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati katika hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika Simba SC  wameng’ara nyumbani baada ya kuichapa bao 1-0 Wydad Casablanca Athletic mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Shujaa wa Simba SC ni Mshambuliaji hatari katika Michuano hiyo  Jean Baleke alifunga dakika ya 30 na bao hilo liliwapeleka wenyeji Mapumziko wakiwa wanaongoza.

Kwa ushindi huo Simba SC wataenda nchini Morocco katika marudiano wakiwa na bao moja hivyo kwenda kutafuta bao jingine au sare ili waweze kutinga hatua ya Nusu Fainali Aprili 29 watarudiana tena.

Wawakilishi katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika timu ya Yanga SC watashuka dimbani kesho kucheza na Rivers United  nchini Nigeria

About the author

mzalendoeditor