Featured Kitaifa

VITUO YA TEHAMA KWA JAMII KUTENGENEZA AJIRA

Written by mzalendoeditor

Vimejengwa na UCSAF Visiwani Zanzibar

Jumla ya wakazi 3,708 Visiwani Zanzibar, wengi wao wakiwa vijana wamepata elimu ya kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano inayotolewa katika vituo vilivyojengwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF) visiwani humo.

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi( SMZ) Dkt Mzee Mndewa.

Amesema vituo hivyo vimejengwa kwa lengo la kupeleka elimu ya TEHAMA kwa wananchi ili kuwawezesha kushiriki katika uchumi wa kidigitali kwa kutumia TEHAMA.

Amesema, ni muhimu kuwajengea uwezo wananchi ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kidigitali.

Vijana wenye uelewa wa TEHAMA hujitolea kufundisha wenzao elimu anbayo inaweza kuwasaidia kujiajiri kwa kufungua sehemu za kutoa huduma za kuprinti, kutoa photocopy, kutengeneza kadi za matukio mbalimbali kwa kutumia program za kompyuta kama vile Microsoft word, adobe na publisher.

Ikiwa ni katika kutekeleza jukumu la kuhamasisha utoaji wa huduma bora katika viwango nafuu, na kuhakikisha kuwa teknolojia ya habari na mawasiliano inapatikana vijijini na sehemu za mijini zenye mawasiliano hafifu kwa bei nafuu. UCSAF imejenga vituo 11 vya TEHAMA kwa jamii Visiwani Zanzibar ambapo vituo 7 vimejengwa Unguja na vituo vinne vimejengwa Pemba.

About the author

mzalendoeditor