Featured Michezo

SIMBA SC YAIKANDA YANGA SC MBIO ZA UBINGWA BADO NGOMA MBICHI

Written by mzalendoeditor

Na.Alex Sonna

SIMBA SC  wameendelea kupunguza gape la Pointi dhidi ya  Yanga SC na kuendelea na mbio za Ubingwa  baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0  mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba SC walianza kwa kasi ya ajabu na mnamo dakika ya 2 Beki Kisiki Henock Inonga aliwanyanyua mashabiki wake akifunga bao safi kwa kichwa akimalizia Krosi ya Shomari Kapombe.

Baada ya kupata bao hilo Simba waliendelea kuishambulia Yanga na dakika ya 32 Kiungo mshambuliaji aliyekubarika kwa mashabiki Kibu Denis alipigilia msumari wa pili kwa shuti kali lililomshinda Diarra.

Kwa ushindi huo Simba wamefikisha Pointi 63 na kupunguza gape la Pointi na kubaki  alama tano huku kila timu ikibakiwa na mechi nne Ligi imalizike.

Yanga wanabaki na Pointi zao 68  ili wawe mabingwa wa Ligi msimu huu wanahitaji kushinda  mechi tatu ili wafikishe Pointi 76 ambazo Simba akishinda mechi zake  zote atakomea pointi 75 .

About the author

mzalendoeditor