Featured Kitaifa

TAMISEMI YATANGAZA AJIRA MPYA ZA UALIMU NA AFYA

Written by mzalendoeditor

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angellah  Kairuki ,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Aprili 12,2023 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa  kuhusu tangazo la nafasi za ajira kwa kada za Ualimu na Afya nchini.

Na.Alex Sonna-DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa kibali cha kuajiri watumishi 21,200 wa Kada za ualimu na Afya.

Hayo yameelezwa leo Aprili 12, 2023   na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angellah  Kairuki  wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jijini Dodoma

Amesema Idadi ya watumishi watakaoajiliwa katika Kada za Ualimu ni 13,130 ambao watafundisha katika shule za Msingi a Sekondari.

Aidha, Waziri Kairuki ameeleza kuwa idadi ya watumishi watakoajiliwa katika kada za Afya ni 8,070 ambao watafanya kazi katika Hospitali za Halmashauri, Vito vya Afya na Zahanati.

Waziri Kairuki amesema waombaji wanatakiwa kuomba ajira kuanzia leo April 12, hadi 25,2023 saa 5:59 usiku.

”Waombaji wote wanatakiwa kuwa na sifa za jumla kama zifuatazo awe mtanzania,awe na ukomo wa umri miaka 45 cheti Cha taaluma,cheti Cha kidato Cha sita na kitambulisho Cha NIDA.”amesema Waziri Kairuki 

Aidha amewataka waombaji  kuepuka utapeli utakaojitokeza wakati wa kuomba nafasi hizo.

About the author

mzalendoeditor