Featured Michezo

SIMBA SC YAIFUATA AZAM FC NUSU FAINALI ASFC BALEKE APIGA HAT TRICK

Written by mzalendoeditor

TIMU ya Simba SC  imeifuata Azam FC katika  Hatua ya Nusu Fainali Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuichakaza mabao 5-1 Ihefu SC kutoka  jijini Mbeya mchezo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Jean Baleke matatu dakika za pili, 16 na 28 na viungo, Mrundi Saido Ntibanzokiza dakika ya 40 na Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 90
na ushei, wakati bao pekee la Ihefu SC limefungwa na kiungo pia Raphael Daudi Lothi dakika ya 61.
Sasa Simba SC itakutana na Azam FC katika mchezo wa Nusu wa Fainali. Ikumbukwe Azam FC ilitangulia Nne Bora Jumatatu kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar hapo hapo Chamazi.
Timu nyingine ambayo tayari ipo Nusu Fainali na Singida Big Stars iliyoitoa Mbeya City kwa kuichapa 4-1 na yenyewe itakutana na mshindi wa Robo Fainali ya mwisho kesho kati ya mabingwa watetezi, Yanga na Geita Gold.

About the author

mzalendoeditor