Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akitoa maelekezo wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wanaozungukwa na mradi wa uzalishaji kokoto katika Kijiji cha Mundemu Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya Bahi Godwin Gondwe.
Eneo ambalo mradi wa uzalishaji kokoto katika Kijiji cha Mundemu Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma unafanyika na kulalamikiwa na wananchi kuleta changamoto ya kusambaa kwa vumbi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akisindikizwa na Mkuu wa Wilaya Bahi Godwin Gondwe kuelekea kwenye gari kwa ajili ya kuanza ziara ya kukagua na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wanaozungukwa na mradi wa uzalishaji kokoto katika Kijiji cha Mundemu Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa siku 45 kwa wawekezaji wa mradi wa uzalishaji kokoto katika Kijiji cha Mundemu Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma kudhibiti vumbi linalosambaa na kusababisha kero kwa wananchi.
Pia ametoa muda huo kwa wawekezaji hao kuhakikisha wananchi hao wanalipwa fidia ili waweze kuondoka na kupisha mradi huo vinginevyo utasitishwa kuendelea na shughuli zake.
Dkt. Jafo ametoa maagizo hayo Aprili 04, 2023 wakati wa ziara ya kikazi kwa lengo kukagua na kujioenea hali halisi, kujadili hatua stahiki zinazofaa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wanaozungukwa na mradi huo.
Akziungumza wakati wa ziara hiyo amesema kuwa Serikali inathamini uwekezaji unaofanywa hapa nchini lakini haitavumilia kuona wananchi wawekezaji wanakiuka sheria ya mazingira hivyo wananchi kupapata madhara.
“Nimepata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wakililamika kupata vumbi kutokana na shughuli inayofanyika hapa na tume iliundwa hapa na watu wa madini na kutoa maelekezo lakini hawakufuata sasa hatuwezi kuvumilia watu hawa hawafuati sharia za nchi, maelezo yangu ni hayo mawili vingine mradi huu utafungwa,” alisisitiza.
Hivyo, kutokana na malalamiki ya wananchi kuhusu milipuko ya barudi wakati wa kuoasua miamba alisema hilo liko chini ya sekta ya madini hivyo alitoa wito kwa wataalamu wa madini kufika na kufuatilia changamotio hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi Godwin Gondwe alisema alimshukuru Waziri Jafo kwa kufika katika eneo hilo na kusikiliza na kushughulikia changamoto hizo.
Aliahidi kuyasimamia maelekezo aliyotoa ili na kuhakikisha wawekezaji hao wanatekeleza maelekezo hayo ndani ya siku 45 ambazo Waziri Jafo ametoa ili kuhakikisha madhara ya vumbi hayawafikii wananchi.
Awali baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wakiwemo Diwani wa Kata ya Mundemu Stanley Mtati, Bw. Richard Nyagani walisema wamekuwa wakipata kero ya milipuko inayotumika kulipua mawe ambayo inaletea madhara yakiwemo kuharibika kwa nyumba.
Hivi karibuni Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)- Kanda ya Kati kwa kushirikiana na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi – Dodoma na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Bahi ilifanya Ukaguzi katika eneo la mradi huo.