Jeshi la Polisi Mkoa wa mwanza linapenda kutoa taarifa kwamba mnamo tarehe  01.04.2023 muda wa saa 20:00 Usiku huko kitongoji cha Kasuzu, kijiji na kata ya  Namagondo, tarafa ya Mumulambo wilayani Ukerewe, mwanaume aitwaye  Anselumu Sebuka, miaka 42, Mkulima na mkazi wa Namagondo, alikutwa  ndani ya chumbachake akiwa amejaribu kujiua kwa kukata uume wake kwa  kutumia kisu chenye ncha kali. 

Inadaiwa Ansele Sebuka alikuwa anatuhumiwa na ndugu zake kuiba mali  mbalimbali za familia yake na za jamii inayomzunguka na kwenda kuziuza pamoja  na ulevi uliokithili ambapo waliamua kumtenga kutokana na tabia zake mbaya.  Baada ya tuhuma hizo ndipo aliamua kujikata uume wake kwa kisu na kuacha  unaning’inia kwa lengo la kujiua. Chanzo cha tukio hilo ni ugonvi wa kifamilia  uliopelekea mhanga kupata msongo wa mawazo. 

Ansele Sebuka alipelekwa katika Hospitali ya wilaya ya Ukerewe kwa ajili ya  matibabu na hali yake inaendelea vizuri. Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi  kufuata njia sahihi za kutatua matatizo yao hususani kuwaona wataalamu wa afya  ya akili ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na msongo wa  mawazo na kukosa uvumilivu wa migogoro mbalimbali katika jamii. 

  

Tarehe 03.04.2023 majira ya saa 12:00 mchana, kuliripotiwa tukio la mauaji ya  Milembe Mihayo, miaka 11, mkazi Sumaha, baada kupigwa na baba yake mzazi  siku ya tarehe 27.03.2023 majira ya saa 08:00 asubuhi katika kitongoji cha Ishungi  kata ya Wala Wilayani Kwimba.

1 | P a g e 

Baada ya kulipotiwa kwa taarifa hiyo, Jeshi la Polisi lilifatilia kwa haraka na  kufanikiwa kumkamata Mathayo Mishaka, miaka 40, Mkulima na mkazi wa  kijiji cha Sumaha. Baada ya mahojiano ya kina na mtuhumiwa huyo alikiri  kuhusika na mauaji ya binti yake kwa kumchapa na fimbo sehemu za mwili wake  baada ya kumkuta nyumbani kwa babu yake mdogo aitwaye Dotto Masanyiwa akikokuwa ameagizwa, wakiwa bafuni na mvulana aliye kimbia baada ya  kufumaniwa wakiwa wamevua nguo wakitaka kufanya mapenzi ndipo  alipomkamata binti yake na kuanza kumpiga. 

Milembe Mihayo aliendelea kupata maumivu makali bila kupelekwa Hospitali,  ndipo baba yake huyo mzazi akamuagiza mke wake mdogo aitwaye Sofia  Mashaka, Miaka 20, amkande miguu binti huyo iliyokuwa imevimba kutokana na  kipigo na mama huyo alipomuuliza mmewe kuhusu tatizo hilo, alimueleza kuwa 

binti huyo huwa anasumbuliwa na tatizo la miguu kitendo ambacho mama huyu  hakulizika nacho kwani alikuwa ameishi na binti huyo kwa muda wa mwaka  mmoja bila kuona tatizo hilo. 

Mwili wa Milembe Mihayo umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa ndugu kwa  taratibu za mazishi na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo  baada ya kukamilishwa kwa upelelezi. 

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wazazi na walezi kuacha kutoa adhabu za kikatili  kwa watoto wao badalayake watumie njia sahii ya kuwaonya pindi wanapokose ili  kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza. Pia, linawaomba kuendelea  kushirikiana kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili ziweze kufanyiwa kazi  kwa haraka. 

  

Imetolewa na;-  

Wilbroad W. Mutafungwa- SACP  

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.

Previous articlePATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO APRILI 5,2023
Next articleWAZIRI JAFO ATOA MAELEKEZO KUDHIBITI VUMBI UCHIMBAJI KOKOTO BAHI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here