
Chama cha Wafanyakazi Serikali za Mitaa (TALGWU), tawi la RUWASA, kimefanya mkutano mkuu wa uchaguzi wa viongozi wapya ambapo Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Mhandisi Rashid Abdallah, amefanikiwa kutetea nafasi yake ya uenyekiti.
Uchaguzi huo ulifanyika Aprili 24, 2026 jijini Dodoma, katika mazingira ya uwazi na ushirikishwaji mpana wa wanachama, waliotekeleza haki yao ya kidemokrasia kwa kuchagua viongozi watakaoongoza tawi hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Katika uchaguzi huo, viongozi waliochaguliwa ni pamoja na Mhandisi Rashid Abdallah (Mwenyekiti wa Tawi), Ibrahim Fungo (Katibu wa Tawi), Tumaini Gwatalile (Mwenyekiti wa Makundi Maalum – Wanawake), Ashura Nkunya (Katibu wa Makundi Maalum – Wanawake), Victoria Charles (Mjumbe wa Makundi Maalum – Vijana), na Adam Suleiman (Mjumbe wa Makundi Maalum – Watu wenye Ulemavu).
Uongozi huo mpya unatarajiwa kuimarisha mshikamano miongoni mwa wanachama, kulinda na kutetea maslahi yao, pamoja na kuendeleza maendeleo ya chama katika tawi la RUWASA.








