Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI NA MABADILIKO YA MABALOZI WAWILI

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan  amefanya mabadiliko ya vituo kwa Mabalozi wawili (02) na uteuzi wa Balozi  mmoja (01) kama ifuatavyo: 

  1. Amempangia Balozi Humphrey Herson Polepole kuiwakilisha  Tanzania nchini Cuba. Kabla ya uteuzi huu Balozi Polepole alikuwa  Balozi wa Tanzania, nchini Malawi. 
  2. Amemteua Balozi Lt. Jenerali (mstaafu) Yacoub Mohamed  kuiwakilisha Tanzania katika Falme za Kiarabu (UAE). Kabla ya  uteuzi huu, Balozi Mohamed alikuwa Balozi wa Tanzania nchini  Uturuki. 

Uteuzi na kupangiwa Kituo 

  1. Amemteua Bw. Iddi Seif Bakari kuwa Balozi na kumpangia Ubalozi  nchini Uturuki. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Bakari alikuwa Konseli  Mkuu, Dubai. 

Tarehe ya uapisho wa Balozi Bakari itatangazwa baadae. 

Zuhura Yunus 

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

About the author

mzalendoeditor