Featured Kitaifa

NAIBU WAZIRI KIPANGA ATAKA MKANDARASI KUONGEZA KASI UJENZI JENGO LA TAEC DAR ES SALAAM

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga amemtaka Mkandarasi Group Six International Limited kuongeza kasi ya ujenzi katika mradi wa Maabara, Ofisi na Mtambo wa Kinururisho Jumuishi -Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Kanda ya Mashariki.

Mhe. Kipanga ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara kukagua mradi huo.

Amesema pamoja na ubora wa kazi inayoendelea ni vizuri kazi hiyo ikakamilika kwa wakati ili majengo hayo yaweze kutumika kwa kazi zilizokusudiwa.

“Ninawapongeze Tume kwa usimamizi mzuri wa kazi ninaona kazi nzuri, nasisitiza kuongeza kasi ili kazi ikamilike kwa wakati,”amesema Mhe. Kipanga.

Mradi wa ujenzi wa Maabara, Ofisi na Mtambo wa Kinururisho Jumuishi -Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Kanda ya Mashariki unatekelezwa na Mkandarasi Group Six International Ldt kwa gharama ya Shilingi Bilioni 7.9 katika eneo la Mbezi Msakuzi, Dar es Salaam

About the author

mzalendoeditor