Featured Kitaifa

KAMATI YARIDHIA MPANGO NA BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakati akiwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24, Bungeni, Jijini Dodoma, leo tarehe 22 Machi, 2023.

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe Mhe. Fatuma Toufiq akieleza jambo wakati wa kikao hicho.

Sehemu ya Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakifuatilia maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe Mhe. Fatuma Toufiq (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24, kilichofanyika Bungeni, Jijini Dodoma leo Machi 22, 2022.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu akichangia jambo wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24 kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni, Jijini Dodoma.

Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Mariam Kisangi akichangia hoja wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa mwaka wa fedha 2023/24 kilichofanyika Bungeni, Jijini Dodoma leo Machi 22, 2022.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na menejimenti ya ofisi hiyo Bungeni, Jijini Dodoma leo Machi 22, 2022.

PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

Na: Mwandishi Wetu – DODOMA

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imepitisha Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Kikao cha kamati hiyo kimefanyika leo Machi 22, 2023 chini ya Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq ambapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameiongoza Menejimenti ya Ofisi hiyo kuwasilisha mpango na bajeti ya ofisi hiyo.

About the author

mzalendoeditor