Featured Kitaifa

KIMBISA AZITAKA KAMATI ZA SIASA ZA KATA KUJIPANGA KWA USHINDI CHAGUZI ZINAZOKUJA

Written by mzalendoeditor

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mkoa wa Dodoma Alhaj Adam Kimbisa,akizungumza na kamati ya siasa ya kata ya Kiwanja cha Ndege katika muendelezo wa utaratibu wake wa kukutana na kamati za siasa za Dodoma leo Machi 2,2023 jijini Dodoma.

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mkoa wa Dodoma Pili Mbanga,aakizungumza wakati wa kikao cha kamati ya siasa ya kata ya Kiwanja cha Ndege leo Machi 2,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mkoa wa Dodoma Alhaj Adam Kimbisa amezitaka Kamati za Siasa za Kata kujipanga kwa ushindi kwenye chaguzi zinazokuja kwa kuwa wamoja na kutibu vidonda vilivyopatikana waakti wa chaguzi zilizopita.

Kimbisa ametoa maelekezo hayo Machi 2,2023,Jijini Dodoma wakati akizungumza na kamati ya siasa ya kata ya Kiwanja cha Ndege katika muendelezo wa utaratibu wake wa kukutana na kamati za siasa za Dodoma.

“Kupata ushindi hakuna miujiza,ni kujipanga ,kuwa wamoja na kutibu vidonda vilivyopo, mimi siwezi kuona chama kinazama kwa sababu ya mtu mmoja au wawili, mimi nahitaji kura,mkiniuliza unataka nini kwanza nitakwambia kura ,pili nitakwambia kura na tatu nitakwambia kura,sina mahitaji mengine,”alisema.

Kimbisa aliwataka pia kujipanga kuongeza wanachama kwa kuwafikia wageni waliopo waliotokana na ujio wa serikali Dodoma.

“Dodoma ndio Makao Makuu,tumepata wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali nchini,wafanyakazi na wafanyabiashara,kwenye kata zenu mlizoea kuona madaftari yana wanachama wale wale lakini hali imebadilika,

“Hili ni jukumu letu sisi kwenye kata kujiuliza tunawafikiaje,tunawaonaje na tunawashawishi vipi wageni kama sio wanachama waweze kujiunga na chama,”aliongeza.

Awali,Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbanga alisema tayari Mwenyekiti ameshakutana na kamati za siasa za Kata ya Chang’ombe,Viwandani na Nkuhungu lengo likiwa ni kujipanga ili kuhakikisha chama kinashinda katika chaguzi zote zinazokuja wa serikali za mitaa 2024 nna uchaguzi mkuu 2025.

About the author

mzalendoeditor