Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AWATAKA VIONGOZI KUTEKELEZA NA KUSIMAMIA MAJUKUMU YAO

Written by mzalendoeditor
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wengine wa Serikali kabla ya kufungua Mkutano wa Faragha wa viongozi hao uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Machi, 2023.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Mhandisi Zena Said, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella pamoja na Mawaziri mara baada ya kufungua Mkutano wa Faragha wa viongozi hao uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi kutoka Zanzibar Mhandisi Zena Said, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella pamoja na Naibu Mawaziri mara baada ya kufungua Mkutano wa Faragha wa viongozi hao uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi kutoka Zanzibar Mhandisi Zena Said, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella pamoja na Makatibu Wakuu mara baada ya kufungua Mkutano wa Faragha wa viongozi hao uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi kutoka Zanzibar Mhandisi Zena Said, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella pamoja na Naibu Makatibu Wakuu mara baada ya kufungua Mkutano wa Faragha wa viongozi hao uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Machi, 2023.
Viongozi mbalimbali wakiwemo, Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu pamoja na Watoa Mada wakiwa kwenye Mkutano wa Faragha uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Machi, 2023.
 
************************
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi kukumbushana misingi ya uongozi na taratibu za utendaji kazi Serikalini kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo.
 
Rais Samia amesema hayo leo wakati akifungua Mkutano wa Faragha (Retreat) wa Mawaziri na Makatibu Wakuu uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC).
 
Aidha, Rais Samia ametoa wito kwa Viongozi hao kuwa na uelewa wa pamoja wa mtazamo na mwelekeo wa Serikali juu ya masuala mbalimbali.
 
Vile vile, Rais Samia amewataka Viongozi hao kutumia Mkutano huo kukumbushana na kuelekezana juu ya kutimiza ipasavyo wajibu walionao na dhamana walioibeba ya kuwatumikia wananchi.
 
Rais Samia pia amesema umakini na umahiri unahitajika kwa Viongozi katika kutumia na kusimamia rasilimali watu, vifaa na fedha za umma pamoja na kuwa na mipango na mikakati thabiti ya kutekeleza na kusimamia majukumu yao.
 
Kwa upande mwingine, Rais Samia amewataka Viongozi hao kuyasemea mafanikio ya Serikali yaliyopatikana na kuwa wepesi kusahihisha kwa wakati upotoshaji unaofanywa dhidi ya Serikali kupitia watumishi na vitengo vya Habari vya wizarani.
 
Mkutano huo ambao unafanyika kwa mara ya kwanza tangu Rais Samia aingie madarakani, una lengo la kuwakumbusha Viongozi kuhusu dhana ya uongozi na sifa za kiongozi bora na utaratibu wa utoaji wa maamuzi ya kisera ndani ya Serikali.

About the author

mzalendoeditor