Featured Kitaifa

UBAGUZI NA KUKOSEKANA KWA USAWA VINARUDISHA NYUMA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI NCHINI

Written by mzalendoeditor

 

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akizungumza leo Machi 1,2023 jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Unyapaa na Ubaguzi yanayofanyika Machi Mosi kila Mwaka .

MAKAMU Mwenyekiti kutoka Baraza la Watu wanaoishi na VVU _NACOPHA Bw.Yusufu Marere,akisoma risala  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Unyapaa na Ubaguzi yanayofanyika Machi Mosi kila Mwaka  yaliyofanyika leo Machi 1,2023 jijini Dodoma.

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji TACAIDS Bw. Jumanne Issango,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Unyapaa na Ubaguzi yanayofanyika Machi Mosi kila Mwaka  yaliyofanyika leo Machi 1,2023 jijini Dodoma.

MWAKILISHI wa UNAIDS Dkt.Grace Mallya,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Unyapaa na Ubaguzi yanayofanyika Machi Mosi kila Mwaka  yaliyofanyika leo Machi 1,2023 jijini Dodoma.

SEHEMU ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Mkuu  wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Unyapaa na Ubaguzi yanayofanyika Machi Mosi kila Mwaka yaliyofanyika leo Machi 1,2023 jijini Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kuzungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Unyapaa na Ubaguzi yanayofanyika Machi Mosi kila Mwaka yaliyofanyika leo Machi 1,2023 jijini Dodoma.

Na. Alex Sonna-DODOMA  

TANZANIA  imeungana na nchi nyingine Duniani kuadhimisha Siku ya Kupinga Unyanyapaa na Ubaguzi Duniani yanayoadhimishwa kimataifa Machi Mosi kila mwaka ili kuendelea kuangazia na kupaza sauti juu ya kupinga na kupiga marufuku vitendo vyote vya unyanyapaa.

Madhimisho hayo yamefanyika leo Machi 1,2023 Jijini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi katika kuadhimisha siku hii alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) George  Simbachawene.

Kupitia hotuba yake Simbachawene amesema kuwa ubaguzi na kukosekana Usawa na Haki ni miongoni mwa makundi mbalimbali ya kijamii yanayosababisha vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili.

Mhe Simbachawene amesema  Dhana na vitendo vya Ubaguzi vinavyoashiria Ukatili na kutokuwepo kwa usawa vinasababisha kutotimia kwa malengo yetu ya kitaifa ya mwitikio wa VVU na UKIMWI na kurudisha nyuma jitihada za Serikali za kutokomeza UKIMWI.

“Kauli mbiu ya mwaka huu ni “TOKOMEZA UBAGUZI, OKOA MAISHA ambapo inatutaka kuangalia umuhimu wa kuhakikisha tunatokomeza ubaguzi na unyanyapaa miongoni mwa watu wanaoishi na VVU na makundi mengine.

Aidha ameeleza  kuwa kukosekana kwa usawa, uwepo wa mila zilizopitwa na wakati, ubaguzi, kutengwa na unyanyapaa kwa namna mbalimbali vyote hivi vinachangia kasi ya maambukizi mapya ya VVU.

Ameeleza kuwa Takwimu zinaonyesha usawa wa kijinsia, mila hatarishi na ukatili ni wanawake na wasichana ndio wahanga wakubwa.

“Baadhi ya wanawake na wasichana wamepata maambukizi ya VVU kutokana na ukatili wa kingono, Wanawake wenye VVU wapo katika hatari ya ukatili hasa baada ya kuweka wazi hali zao za maambukizi”amesema

Kadhalika, amesema tabia, mila na desturi  hatarishi vimepelekea kukosekana kwa usawa wa kijinsia na ukatili wa kijinsia Tanzania, hali hiyo inachochea na kuongeza kiwango cha maambukizi na baadhi ya matukio yanayosababisha kuambukizwa na kusambaza VVU, kati ya wanawake na wasichana.

Vile vile, amesema  wanawake wameathirika zaidi kutokana na hali ya kutokuwepo kwa usawa katika uhusiano wa kijinsia na majukumu ya kijinsia pamoja na kutopewa fursa ya kufanya maamuzi.

“Ikiwa ni pamoja na kutokuwa na uwezo wa kujadili juu ya matumizi ya kondomu na ngono salama, vipengele hivi husababisha ukiukwaji wa haki za binadamu na ukatili wa kijinsia”amesema

Hata hivyo amesema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Baraza la NACOPHA wameweza kufanikisha kuhamasisha watu wanaoishi na VVU kujiunga kwenye konga ambapo hushirikiana pamoja kujikwamua kiuchumi, kupeana taarifa mbalimbali, na hata kuhudumiana..

“Nachukua fursa hii kuwapongeza wadau wote na mashirika yanayotoa msaada kwa watu wanaoishi na VVU na watoto yatima. Aidha nawapongeza TACAIDS na Baraza la watu wanaoishi na VVU kwa kuendelea kusimamia maslahi pamoja na haki za ustawi wa watu wanaoishi na VVU nchini”amepongeza   Simbachawene 

Pia amesema Serikali imehakikisha Dawa za ARV zinaendelea kupatikana nchini bila kikwazo chochote, hivyo wale wote wanaogundulika kuwa na VVU waanze na waendelee kutumia ARV kama inavyooelekezwa na wataalamu wa Afya.

“Natoa rai kwa watoa huduma wote kuepuka vitendo vya kunyanyapaa na lugha za kudhalilisha WAVIU pindi wanapohitaji kuhudumiwa. Suala hili la unyanyapaa na ubaguzi linarudisha nyuma jitihada za kuutokomeza UKIMWI”, amesisitiza Simbachawene

Simbachaene amesema kuwa Serikali ya Tanzania imeweka sera na mifumo mizuri ya kisheria, mipango ya kitaasisi na miongozo ya kitaifa ambayo imetengeneza mazingira mazuri ya kuboresha haki za binadamu, usawa wa kijinsia pamoja na ushirikiano wa jamii.

Kupitia Wizara ya Jinsia Wanawake na watoto mwaka 2000 serikali ilitunga Sera ya Maendeleo ya Wanawake na jinsia na mpango mkakati wa kijinsia ili kuhamasisha usawa wa kijinsia na ushirikishwaji wa jamii.

Sera hiyo pia inaongelea kuhusu unyanyasaji wa wanawake na watoto kupitia mkakati wake wa kijamii kwa ajili ya kuwalinda wanawake na watoto dhidi ya maambukizi ya VVU.

Naomba kutoa wito kwa TACAIDS na wadau wake kuangalia jinsi gani mnaweza kuandaa jumbe kwa makundi yote ikiwemo matumizi ya maandishi ya nukta nundu kutoa elimu kwa kundi hili.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa NACOPHA Bw. Yusuph Marere, amesema Katika maadhimisho hayo wanaungana na wenzao duniani kote kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa kuzingatia heshima na utu wa binadamu pasipo kuwa na ubaguzi wa aina yoyote.

“Siku hii muhimu inatukumbusha kuwa kila mmoja anapaswa kuheshimu na kuheshimiwa na vilevile inatukumbusha kuwa na mifumo, sera na huduma jumuishi zinazohusisha makundi yote katika jamii na pia tunakumbushwa kupinga aina zote za unyanyapaa na ubaguzi kwa WAVIU na watu walio katika makundi maalumu”,amesema Bw.Marere

Ameeleza kuwa kwa kiasi kikubwa unyanyapaa na ubaguzi katika jamii umechangia watu wengi kushindwa kujitokeza ili kupata huduma bora za VVU na UKIMWI ikiwemo upimaji wa hiari wa VVU, tiba na matunzo.
Amesema Juhudi za dhati zinahitajika ili kukomesha hali hii katika taifa letu na kwa kufanya hivyo tunaweza kufikia malengo ya dunia ya kutokomeza UKIMWI ifikapo 2030.

About the author

mzalendoeditor