Featured Kitaifa

TARURA NA TANROADS DODOMA ZATAJA MAFANIKIO KATIKA KIPINDI CHA AWAMU YA SITA

Written by mzalendoeditor

Na Mwandishi Wetu-DODOMA

Sekta ya Miundombinu ya Barabara imeendelea kuimarika kupitia Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na TANROADS Mkoa wa Dodoma hasa katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na uboreshaji mkubwa wa barabara tofauti na kipindi cha nyuma.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mkapa katika muendelezo wa vipindi maalumu vya kutangaza Mafanikio Serikali ya Awamu ya sita kwa TARURA Mkoa wa Dodoma.

Amesema kubwa kwa Mkoa wa Dodoma katika miundombinu ni ujenzi wa Barabara za mzunguko zenye urefu wa kilometa 112 ambapo LOT 1 inatoka Nala-Veyula-Mtumba-Ihumwa yenye urefu wa Km52.3 Ujenzi huu unagharimu Shillingi Milioni 100.84 na LOT 2 yenye urefu wa Km 60 inayotoka Dry pot Ihumwa, Ngo’ngo’na, Matumbulu, Bihawana -Nala, Ujenzi unaogharimu Shillingi Milioni 120.8. Ujenzi wa Barabara za mzunguko utagharimu Shilingi Milioni 221 kwa LOT zote mbili.

“Mradi huu ni wa aina yake barani Afrika tunampongeza sana Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa fedha za kukamilisha ujenzi wa kilomta 112.3 Km za barabara za mzunguko ndani ya Mkoa wa Dodoma ” amesisitiza Mhe. Senyamule.

Kwaupande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Lusako Kilembe ameelezea mafaniko yaliopatika na matarajio kwenye taasisi hiyo katika kipindi cha miaka miwili.

Akizungumza na waandishi wa Habari,Leo Frebruari 23,2023 Makao makuu ya mkoa Dododma ameelezea Mkoa wa Dodoma unahudumia mtandao wa barabara wenye jumla ya urefu wa km 7540.94 ambapo km 2702.11 ni barabara za Makusanyo (Collector roads), km 4004.003 ni barabara za Mlisho (Feeder roads) na km 834.035 ni barabara za Jamii (Community roads).

Hata hivyo ameelezea Sehemu kubwa ya mtandao huu ni ya tabaka la udongo na changarawe ambapo sehemu hii ina jumla ya urefu wa Km 7238.584 sawa na asilimia 95.99 ya mtandao wote wa barabara lakini barabara zilizopo katika tabaka la lami na zege ni km 302.356 sawa na asilimia 4.01 tu ya mtandao wote wa barabara.

“wakala wa Barabara mkoa wa Dododma unahudumia mtandao wa barabara wenye jumla ya urefu wa km 7540.94 ambapo km 2702.11 ni barabara za Makusanyo (Collector roads), km 4004.003 ni barabara za Mlisho (Feeder roads) na km 834.035 ni barabara za Jamii (Community roads).

“lakini pai tunatekeleza Sehemu kubwa ya mtandao huu ni ya tabaka la udongo na changarawe ambapo sehemu hii ina jumla ya urefu wa Km 7238.584 sawa na asilimia 95.99 ya mtandao wote wa barabara lakini barabara zilizopo katika tabaka la lami na zege ni km 302.356 sawa na asilimia 4.01 tu ya mtandao wote wa barabara,”amesema

Pia ameelezea Katika utekelezaji wa miradi ya barabara kwa mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya shillingi Billioni 55.60 zilitengwa kwa ajili ya matengenezo na ukarabati wa miradi, ikiwemo miradi mikubwa ya maendeleo (development Projects) na
bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022 imeongezeka kutoka Shilingi
Billioni 12.40 hadi Shilingi Bilioni 55.60. Kiwango hicho ni sawa na ongezeko la bajeti asilimia 348.39.

Aidha Katika utekelezaji wa miradi ya barabara kwa mwaka wa fedha 2022/2023 jumla ya shillingi Billioni 8 zimetengwa kwa ajili ya Ujenzi wa barabara za nyongeza za mji wa serikali na fedha maalum kiasi cha Shilingi Bilioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa barabara katika eneo la Nala Viwandani km 5.

“Katika utekelezaji wa miradi ya barabara kwa mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya shillingi Billioni 55.60 zilitengwa kwa ajili ya matengenezo na ukarabati wa miradi, ikiwemo miradi mikubwa ya maendeleo (development Projects) na
bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022 imeongezeka kutoka Shilingi
Billioni 12.40 hadi Shilingi Bilioni 55.60. Kiwango hiki ni sawa na ongezeko la bajeti asilimia 348.39.

“mkoa wa Dodoma miradi ya barabara kwa mwaka wa fedha 2022/2023 jumla ya shillingi Billioni 8 zimetengwa kwa ajili ya Ujenzi wa barabara za nyongeza za mji wa serikali na fedha maalum kiasi cha Shilingi Bilioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa barabara katika eneo la Nala Viwandani km 5,”amesema Kilembe.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika mkoa wa Dodoma imejipanga kuhakikisha kuwa miradi inayotekelezwa inakamilika kwa kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kazi zifanyike kwa ubora na kuleta thamani ya fedha iliyokusudiwa (value for money) na kuhakikisha barabara zinapitika wakati
wote.

About the author

mzalendoeditor