Featured Kitaifa

e-GA YAZIUNGANISHA OFISI ZOTE ZA SERIKALI ZINAHUSIKA NA UKUSANYAJI MAPATO

Written by mzalendoeditor

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka  ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Februari 23,2023 jijini Dodoma  wakati akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo.

Na.Alex Sonna-DODOMA

KUTOKANA  na kuwepo kwa mifumo mingi ya ukusanyaji kodi na taarifa za serikali katika mfumo wa kifedha nakusababisha upotevu wa mapato, Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) imeziunganisha ofisi zote za serikali zinazohusika na ukusanyaji wa mapato ili kuona mlolongo wa shughuli za makusanyo zinazofanywa na kudhibiti mianya yote ya upotevu wa makusanyo hayo.

Hayo yamesemwa leo Februari 23,2023 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba,wakati  akitoa taarifa ya utekelezaji wa shunghuli mbalimbali za mamlaka hiyo kwa waandishi wa habari.

Mhandisi Ndomba, amesema kuwa  uungwanishaji wa mifumo hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG yakuitaka serikali kuwa na mifumo jumuishi kwa taasisi zake ili kuona mlolongo wa makusanyo na taarifa unavyoenda.

“Mfumo huu umeisadia serikali kuongeza mapato lakini pia kuona kiasi cha fedha ambacho kinakusanywa kila siku kupitia mfumo huu hata muda huu ukitaka kuangalia ni kiasi gani kimeingia unaona moja kwa moja tofauti na ilivyokuwa hapo awali wakati tunatumia vitabu vya stakabadhi”amesema  Mhandisi Ndomba

Hata hivyo amsema  mfumo huo pia unaisadia serikali kutambua ni taasisi gani ambazo zimekuwa zikiongoza kwa ukusanyaji mapato nchini.

“Lakini pia mfumo huu unaisaidia serikali kupata takwimu za kila halmashauri,taasisi na kutambua kuwa ni eneo gani ambalo limekuwa linachangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la taifa”amesisitiza Mhandisi Ndomba

Aidha amesema kuwa katika kuhakikisha wanaijenga Serikali ya Kidijiti, Katika kipindi cha miaka 10 ijayo,itaandaa na kutekeleza mikakati madhubuti ili kuimarisha zaidi utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao.

Mhandisi .Ndomba ameeleza kuwa mikakati hiyo ni pamoja na kuwa Sehemu moja ambayo huduma mtandao zote zitakuwa zinapatikana,Uwezo wa kutumia teknolojia mpya zinazoibuka, hasa zile za akili bandia, sarafu za kidijiti na teknolojia za kifedha, ili kuwezesha maboresho ya kiutendaji katika Taasisi za Umma na utoaji wa huduma kwa Umma.

“Pia Uzalishaji wa vifaa na miundombinu ya TEHAMA (Hardware) ndani ya Tanzania pamoja na Mifumo na miundombinu ya Serikali mtandao iliyobora na imara zaidi,”amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa amesema mifumo ya ukusanyaji mapato kwa njia ya control naomba imesaidia kuokoa fedha ambazo zamani zilikua zikilipwa kwa njia isiyo ya kimatandao.

About the author

mzalendoeditor