Featured Kitaifa

TABIA YA WATUMISHI KUTOTUNZA NYARAKA ZA SERIKALI INA HATARISHA USALAMA WA TAIFA.

Written by mzalendoeditor

 

 NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia elimu Mhe. David Silinde,akizungumza  wakati akifungua Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Sekretarieti za Mikoa na Mmlaka za Serikali leo Februari 23,2023 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Naibu  Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia elimu Mhe. David Silinde (hayupo pichani) wakati akifungua Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Sekretarieti za Mikoa na Mmlaka za Serikali leo Februari 23,2023 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia elimu Mhe. David Silinde,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Sekretarieti za Mikoa na Mmlaka za Serikali leo Februari 23,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

IMEELEZWA kuwa tabia ya baadhi ya watumishi wa Umma kutokuzingatia utunzaji wa nyaraka za Serikali hali hiyo husababisha heshima ya nyaraka za Serikali kutozingatiwa, na kuhatarisha usalama wa Taifa.

Hayo yameelezwa leo FEBRUARI 23,2023 jijini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia elimu Mhe. David Silinde wakati akifungua Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Sekretarieti za Mikoa na Mmlaka za Serikali.

Mhe. Silinde amesema uzoefu unaonyesha utunzaji wa nyaraka za serikali hauzingatiwi kama inavyotakiwa hasa maeneo yanayosimamiwa na Makatibu tawala wasaidizi.

“Watu wanatembea na nyaraka hadharani bila kufunikwa, wengine wanaenda nazo nyumbani pia na kuzitoa wanapokuwa kwenye kumbi za starehe na hivyo kusababisha heshima ya usalama wa nyaraka za serikali kutokuzingatiwa na kuhatarisha ustawi wa taifa letu,”amesema Silinde.

Amewataka kwenda kudhibiti uvujishwaji wa siri za Serikali katika zama hizi za utandawazi mnatakiwa  muwe mstari wa mbele katika kuzitunza.

Hata hivyo amesema ofisi hiyo imeanza kupima utendaji kazi wa wakuu wote wa idara na haitosita kuchukua hatua kwa yeyote mwenye utendaji usio ridhisha.

”Kila halmashauri ihakikishe inaandaa mpango wa kutathimini utendaji kazi, mpango wa mafunzo, utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu na mpango wa Rasilimali watu na kuongeza kuwa hayo ndiyo mambo wanayohitaji kila halmashauri kupanga.”amesema

Pia amewataka watendaji hao kusimamia suala la maadili hasa mavazi kwa kuwaelekeza watumishi kuzingatia Waraka wa Utumishi wa Umma Na.3 wa mwaka 2007 unaohusu mavazi.

Kwa upande wake ,Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI  (Elimu), Dk Charles Msonde.  amesema kikao hicho kitakachofanyika kwa siku tatu kuanzia leo Feb 23-25 kikafanye kasi ya kuwakumbusha na kuelekezana umuhimu wa malengo waliyo yaweka kama nchi ili kuwahudumia wananchi katika maeneo mbalimbali ya Utumishi wao.

Awali  Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa TAMISEMI Bi. Angelista Kihaga amesema kikao hicho kitawasaidia maafisa hao kubadilishana uzoefu, kupata mafunzo yatakayo ongozwa na wataalum kutoka Wizara na Taasisi za Serikali na kuamini kuwa watakapotoka hapo wataenda kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma.

About the author

mzalendoeditor