Featured Michezo

SIMBA SC YAANZA VIBAYA LIGI YA MABINGWA

Written by mzalendoeditor

WAWAKILISHI katika Michuano ya klabu Bingwa Afrika Timu ya Simba SC imeanza vibaya baada ya kuchapwa bao 1-0 na wenyeji Horoya AC mchezo uliopigwa nchini Guinea.

Wenyeji walipata bao dakika ya 18 likifungwa na  Pape N’diaye kwa kichwa akimalizia mpira wa Kona mnamo dakika ya 80 Horoya  walikosa Penalti iliyopanguliwa na Aishi Manula.

Kwa ushindi huo Horoya wameshika nafasi ya pili wakiwa na Pointi tatu sawa na  Casablanca  wakiongoza kwa wingi wa mabao baada ya kuichapa  Vipers SC  mabao 5-0.Simba SC akishika nafasi ya tatu akiwa hana Pointi huku Vipers wakishika Mkia.

About the author

mzalendoeditor