Featured Kitaifa

MAAMBUKIZI MAPYA UGONJWA WA KIFUA KIKUU NCHNI YAPUNGUA KWA ASILIMIA 32 KATI YA ASILIMIA 75

Written by mzalendoeditor

 

KAIMU Meneja Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Peter Neema ,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa  Uzinduzi wa Mapitio ya Muhula wa Kati wa Mpango Mkakati wa Taifa Nchini awamu ya sita uliofanyika leo Februari 10,2023 jijini Dodoma.

MKURUGENZI Msaidizi Sera na Mipango Wizara ya Afya Lusajo Ndagile,akizungumza wakati wa  Uzinduzi wa Mapitio ya Muhula wa Kati wa Mpango Mkakati wa Taifa Nchini awamu ya sita uliofanyika leo Februari 10,2023 jijini Dodoma.

MKUU wa Programu na Uimarishaji Mifumo Wizara ya Afya Dkt.Catherine Joachim,akizungumza wakati wa  Uzinduzi wa Mapitio ya Muhula wa Kati wa Mpango Mkakati wa Taifa Nchini awamu ya sita uliofanyika leo Februari 10,2023 jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Shirika la Shidefa Plus Kutoka Mkoani Shinyanga, Bi. Radia  Khaji akizungumza na waandishi wa habari wakati wa  Uzinduzi wa Mapitio ya Muhula wa Kati wa Mpango Mkakati wa Taifa Nchini awamu ya sita uliofanyika leo Februari 10,2023 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Mapitio ya Muhula wa Kati wa Mpango Mkakati wa Taifa Nchini awamu ya sita uliofanyika leo Februari 10,2023 jijini Dodoma.

KAIMU Meneja Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Peter Neema ,akiwa katika picha ya pamoja wakati wa  Uzinduzi wa Mapitio ya Muhula wa Kati wa Mpango Mkakati wa Taifa Nchini awamu ya sita uliofanyika leo Februari 10,2023 jijini Dodoma.

………………………….

 Na Alex Sonna-DODOMA
KAIMU  Meneja Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Peter Neema,amesema takwimu zinaonesha Maambukizi mapya ya ugonjwa wa kifua kikuu  nchini yamepungungua kwa asilimia 32 kati ya asilimia 75 ambazo zililengwa  kufikiwa ifikapo 2025 ili kupunguza Vifo vitokanavyo na Ugonjwa huo.
Hayo ameyasema leo Februari 10,2023 Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Mapitio ya Muhula wa Kati wa Mpango Mkakati wa Taifa Nchini awamu ya sita ambapo amesema  kuwa wanafanya mkakati wa kuongeza Mashine, Maabara na kutoa elimu kwa ajili ya kupima vina saba vya Kifua Kikuu ili kufikia lengo la Uibuaji wa Ugonjwa huo.
Dk.Neema amefafanua kuwa wanatarajia kufanyia maboresho katika Mpango Mkakati wa Sita ili kuchukuaa hatua zilitolewa katika ripoti na kuwezesha kufikia malengo ifikapo mwaka 2025.
”Sasa hivi tunategemea kufanyia maboreshi katika mpango mkakati wetu wa sita ili kuchukua mapendekezo yaliyotolewa katika ripoti na tuweze kufikia malengo yetu vizuri tutakapofika mwisho wa mpango mkakati huu 2025” amesema Dkt.Neema
Hata hivyo  Dkt.Neema ameeleza changamoto kwenye uibuaji wa maambukizi mapya ya Kifua Kikuu, kutokana wagonjwa wengi kukosa elimu bora  juu ya uibuaji wagonjwa hao.
”Tumekuwa tukipata shida kwenye uibuaji wa maambukizi mapya ya Kifua Kikuu, kutokana wagonjwa wengi kukosa elimu bora  juu ya uibuaji wagonjwa hao hivyo tumejipanga kutoa elimu zaidi kuhusu ugonjwa huo kwa jamii ”amesema
Naye  Mwakilishi wa Shirika la Shidefa Plus Kutoka Mkoani Shinyanga, Bi. Radia  Khaji amesema wanatumia wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii kwenda kutoa Elimu Juu ya Kifua Kikuu
”Tumekuwa tukifanya  uchunguzi wa awali kwa wachimbaji wa Madini wenye dalili za Ugonjwa huo ili kupelekwa kufanyiwa uchunguzi zaidi katika vituo vya kutolea huduma za afya”ameeleza

About the author

mzalendoeditor