Na Gideon Gregory, Dodoma.
WANAOBAKA WATOTO WASIDHAMINIWE
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya ameomba wanaobaka watoto chini ya miaka Kumi wasidhaminiwe kutokana na kuwepo kwa ongezeko kubwa la watoto wadogo kubwakwa.
RPC Mallya ameyasema hayo leo Mei 15,2024 Jijini Dodoma kwenye Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyoambatana na uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili (MTAKUWWA II 2024/25 – 2028/29).
Aidha ameomba kuwepo na nyumba maalum za kuwalea watoto wanofanyiwa vitendo hivyo kama ilivyo kwa waathirika wa madawa ya kulevya kwani tatizo la watoto wengi kuingiliwa limeongezeka na kusababisha matatizo makubwa ya kiafya kwa waathirika hao.
“Wazazi naomba muanze kuwafundisha watoto wenu kufanya kazi za mikono na kuwa na utamaduni wa kuwasikiliza ili kutatua changamoto wanazozipitia huko wanapokuwa kutoana na dunia kwasasa kubadirika,”ameomba RPC Theopista.