Uncategorized

WIZARA YA ELIMU YATANGAZA NAMBA MAALUM ZA KUTOA TAARIFA

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dk.Francis Michael,akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza namba ambazo zitasaidi kupokea malalamiko au taarifa zinazohusu sekta ya elimu nchini   leo Februari 3,2023 Jijini Dodoma,

……………………………….

Na.Alex Sonna-DODOMA
 
 WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanzisha kituo cha huduma kwa wateja (Call center), ambacho kitakuwa kinapokea taarifa mbalimbali kutoka kwa wananchi zinazohusu sekta ya Elimu lengo likiwa ni kufanyiwa kero hizo kwa wakati.
Akizindua namba maalum hiyo  leo Februari 3,2023 Jijini Dodoma,Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dk.Francis Michael amesema kuwa kituo hicho kitasaidia kupata taarifa kwa wakati.
 Dk.Michael amesema kituo hicho kitakuwa wazi kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni na kwamba  mtu, mtanzania yoyote atakayeona jambo ambalo sio jema  ambalo linakiuka miongozo, tamaduni na maadili  kwenye taasisi za elimu, shule za msingi, sekondari pamoja na vyuo atoe taarifa kupitia namba ya mezani  0262160270 na simu ya mkononi 0737962965.
”Kupitia namba hizo tunategemea kupata taarifa zinazohusu malalamiko yanayohusu ukiukwaji wa taratibu na miongozo ya utoaji elimu kwa taasisi hizo za elimu na kwamba wizara hiyo imeona ni vema kuja na kituo cha kutolea taarifa zinazohusu vitendo visivyo vya maadili.”amesema Dk.Michael
Aidha amefafanua  kuwa kama kuna mwananchi yoyote atapata taarifa za vitendo hivyo ambavyo vinaenda kinyume na maadili, miongozo na taratibu za taasisi ya elimu watumie kituo hicho.
“Kama mnavyofahamu siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa kwenye mitandao na magazeti kumekuwa na taarifa ambazo wananchi wamekuwa wakizipata ya upotoshaji wa maadili ya watoto shuleni kwetu pamoja na tabia chafu ambazo zimekuwa zikifanya na baadhi ya taasisi zetu na tulipeleka timu na ripoti hiyo itatolewa hivi karibuni,” amesema.
Pia ameongeza kuwa taarifa zitakazotolewa zitakuwa ni siri na kwamba mtoa taarifa hizo atalindwa kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo  wizara hiyo imezuia Vitabu ambavyo maudhui yake hayaendani na Mila,desturi na utamaduni wa mtanzania katika shule zote zilizopo nchini.
Wizara ilitoa waraka  namba 4 wa mwaka 2014 pamoja na sheria na nyaraka nyingine na miongozo inayohusu elimu ililenga katika kuhakikisha kuwa vitabu vya ziada na kiada vinavyotumika  katika Shule zilizosajiliwa nchini kuhakikisha vinavyotumika ninakuwa na maudhui kulingana na Mila, desturi na utamaduni wa nchi za kumlinda wa kitanzania  mtoto aliyopo shuleni.
Ameeleza kuwa katika kutekeleza wa waraka huo wizara imebani Kuna baadhi ya Shule ambazo zimekuwa zikiingizana kutumika vitabu ambavyo maudhui yake yanakinzana na mila, desturi, miongozo pamoja na tamaduni za mtanzania.
Aidha Dk.Michael amewataka wamiliki wa waendeshaji wa shule za Umma na binafisi zilizosajiliwa nchini kufuata na kuzingatia waraka namba 4 vinginevyo hatua Kali zitachukuliwa pamoja na kufungiwa usajili  zinazoweza kuchukuliwa

About the author

mzalendoeditor