Na Bolgas Odilo-Mzalendo blog
MABINGWA Watetezi Yanga SC wametinga hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa kishindo baada ya kuichapa mabao 7-0 Rhino Rangers kutoka Mkoani Tabora mchezo uliopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga kipindi cha kwanza yamefungwa na Dickson Ambundo dakika ya 7,Kennedy Musonda dakika ya 15,Stephane Aziz Ki dakika ya 19,Farid Mussa dakika ya 24 na Yannick Bangala dakika ya 26.
Kipindi cha pili kilianza tu Kennedy Musonda kupingilia msumari wa sita dakika ya 46 mnamo dakika ya 88 Yanga walikosa mkwaju wa Penalti iliyopigwa na Clement Mzize na dakika ya 90+5 David Bryson alihitimisha bao la saba.
Kwa ushindi huo Yanga SC watakutana na Tanzania Prisons katika hatua ya 16 bora ambao wamewatoa Mashujaa mchezo utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.