Featured Kitaifa

DK.JAFO ASHIRIKI VIKAO VYA MASUALA YA BIASHARA YA HEWA UKAA DUBAI

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzani Dubai baada ya kikao na watendaji wa wakuu wa kampuni ya BLUE CARBON leo Januari 19, 2023.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akisaini kitabu cha wageni alipowasili Ubalozi mdogo wa Tanzania nchini Dubai kabla ya kikao na watendaji wakuu wa kampuni ya BLUE CARBON leo Januari 19, 2023.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzani Dubai baada ya kikao na watendaji wa wakuu wa kampuni ya BLUE CARBON leo Januari 19, 2023.

………………………..

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo,leo ameshiriki vikao mbalimbali vya kubadilishana mawazo katika masuala ya biashara ya hewa ya ukaa Dubai.

Ziara yake ya kikazi imeanziw katika Ofisi ya Ubalozi mdogo uliopo Dubai na kukutana na Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Balozi Iddi Seif Bakari.

Pia Dkt. Jafo amekutana na kufanya kikao na viongozi na watendaji wakuu wa kampuni ya BLUE CARBON ya Dubai.

Ziara hiyo ya kikazi ni mwendelezo wa maelekezo ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuifungua Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiunchumi.

Serikali ya Dkt. Samia kwasasa inaifungua Tanzania katika nyanja pana ya mazingira duniani kwa kupitia biashara ya hewa ya ukaa baada ya Tanzania kuweka muongozo na kanuni za biashara ya Hewa ya Ukaa ambayo inatarajiwa kuongeza pato la Taifa kwa siku chache za usoni na kuiweka Tanzania katika sura nzuri ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendelea na kimazingira kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

About the author

mzalendoeditor