Featured Kitaifa

MHE.JOHARI,DKT.SHEKALAGHE WAJADILI MIKAKATI YA KUIMARISHA UTEKELEZAJI WA SHERIA NCHINI

Written by Alex Sonna

 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe, Ofisini kwake Mtumba, Jijini Dodoma tarehe 23 Julai, 2026.

Pamoja na mambo mengine kikao baina ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu kimelenga kuendeleza zaidi ushirikiano, na kuendelea kuhakikisha utekelezaji bora wa masuala ya Kisheria nchini.

Katika ziara hiyo Dkt. Shekalaghe aliambatana na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma, Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Obadia M. Kameya.

About the author

Alex Sonna