Featured Michezo

SIMBA SC YACHUKUA POINTI 7 KANDA YA ZIWA

Written by mzalendoeditor
 
 
WAKICHEZA Mechi tatu kanda ya Ziwa Timu ya Simba SC imevuna pointi 7 kati ya 9 baada ya kuichapa KMC mabao 3_1 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC  ulipigwa kwenye dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.
 
Simba sc ilianza kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa nahodha wao, John Bocco na kuwatanguliza mbele mpaka mapumziko wakiwa mbele kwa 1-0 kabla ya KMC kusawazisha.
 
Simba Sc ilipata bao la pili kupitia kwa nyota wao Okra na baadae  Henock Inonga akifunga mahesabu kwenye mchezo huo na kufanya matokeo kuwa 3-1.
Kwa Matokeo hayo wamevuna pointi 7 lands ya Ziwa baada ya kuichapa Geita Gold 5_0,Sare ya kufungana bao 1_1 na Kagera Sugar na leo wakiichapa KMC.
Simba wamefikisha Pointi 41 wakibaki nafasi ya pili wakiachwa kwa tofauti ya Pointi 6 na Vinara wa Ligi Yanga wenye Pointi 47.
Mchezo mwingine wenyeji Tanzania Polisi wameshindwa kutamba katika uwanja wa Ushirika Moshi wakilazimishwa sare ya kufungana mabao 3_3 na Coastal Union kutoka jijini Tanga.

About the author

mzalendoeditor