Featured Kitaifa

GGML YAONGOZA TUZO YA UWAJIBIKAJI BORA KWA JAMII

Written by mzalendoeditor
 
KAMPUNI ya Geita Gold Mining Ltd. (GGML) imenyakua tuzo ya juu ya uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii katika Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) wiki iliyopita. 
Aidha, GGML ilipokea tuzo ya juu kwa miradi yake ya uwajibikaji kwa jamii na mshindi wa pili katika kipengele cha muajiri bora wa sekta binafsi.
Kampuni ya AngloGold Ashanti – Geita Gold Mining Limited inajivunia kwamba mafanikio haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na michango ya wafanyakazi wake, wakandarasi, uongozi, na kuendelea kuungwa mkono na kuongozwa vyema na serikali.

About the author

mzalendoeditor