NAIBU Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Deogratius Ndejembi, akifungua kongamano la 13 la mwaka la wataalamu wa ununuzi na ugavi lililofanyika mkoani Arusha.
MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godfrey Mbanyi akiongea katika kongamano la 13 la mwaka la wataalamu wa ununuzi na ugavi.
BAADHI ya wataalamu wa ununuzi na ugavi wakifuatilia jambo katika kongamano lao la 13 la mwaka linaloendelea mkoani Arusha.
………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Naibu waziri wa Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi na utawala bora Deogratius Ndejembi amewataka waajiri wote nchini kuajiri wataalamu wa ununuzi na Ugavi wenye sifa ili kuepusha mzigo wa lawama kwa baadhi yao pindi miradi inapokwama.
Ndejembi alitoa Rai katika kongamano la 13 la mwaka la wataalamu wa ununuzi na ugavi lililofanyikia jijini Arusha ambapo alisema kuwa ili kuepusha hilo ni vyema waajiri wote wakahakikisha wanaweka watu wenye sifa kusimamia idara za ununuzi na ugavi.
“Na panapotokea mwajiriwa kakosa sifa wasisite kuwapeleka shule ili kuweza kujiendeleza wakiwaombea categorization na sisi tutajitahidi kuzifanyia kazi ikiwa lengo ni kupata watu wenye sifa katika sekta hii,”alisema Naibu Ndejembi
Aidha aliitaka bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi kuendelea kuchukua hatua kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanununi zilizopo kwa wataalamu wanao kiuka miiko ya taaluma yao ili kuhakikisha wataaalamu hao wanafanya kazi kwa weledi na ujuzi kwani wanamchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi.
“Ili kuleta tija kwenye utendaji wa miradi serikali lazima ijielekeze katika kufanya ununuzi wa kimkakati kwa kuzingatia ukubwa wa ununuzi na uwiano mfananao wa bidhaa na huduma zinazotumika serikalini ambapo ni imani yangu kwenu kupitia mada na majadiliano mbalimbali zitakazowasilishwa kuhusu ununuzi wa kimkakati zitawajengea uwezo na ufanisi katika katika kutekeleza miradi,”Alieleza.
Alifafanua kuwa serikali ina matumaini makubwa na wataalamu wa ununuzi na ugavi katika kufikia malengo ya mipango ya maendeleo ya taifa ya miaka mitano ambapo anategemea maadhimio ya kongamano hilo yatapelekea kupunguza matatizo yanayotokea katika ununuzi na ugavi.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi (PSPTB) Godfrey Mbanyi alisema kuwa mwaka 2022 wameweza kusajili wataalamu 1995 na kupeleka idadi ya wataalamu kuwa 15309 ambapo wataendelea kuchua hatua madhubuti kwa wataalamu wanaofanya kazi bila kisajiliwa.
“Bodi ipo katika hatua za awali za kuchukua hatua za kinidhamu ambapo imekusudia kuwaita wataalamu 63 ili waweze kutoa maelezo na hatua mbalimbali ziweze kuchukuliwa pamoja na kuchukua hatua za karipio kwa wataalamu 78 ambao wamebainika kufanya kazi chini ya weledi na maelekezo ya kitaaluma,” Alisema Mbanyi.
Aidha alieleza kuwa lengo la kongamano hilo ni kuwaleta na kuwakutanisha pamoja wataalamu wa ununuzi na ugavi ili kujadili fursa na changamoto ambapo ameahidi wataendelea kufanya kazi kwa weledi ili kupeleka taaluma hiyo katika kiwango kinachohitajika na serikali ya awamu ya sita.
Naye mwenyekiti wa bodi hiyo Jacob Kibona alisema kuwa bodi imepewa jukumu la kisheria la kusimamia Wataalamu wa ununuzi na ugavi hii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba nchi yetu inakuwa na wataalamu wa kutosha wenye sofa stahiki na kufuatilia utendaji wao.
Alisema mara nyingi inapotokea changamoto kwenye miradi bila kujali muhisika alihusika katika kusimamia kutekeleza hatua hiyo maafisa ugavi ma ununuzi ndio pekee wanaoshitumiwa ambapo kufanikiwa kwa miradi kunategemea weledi wa ununuzi na ugavi ambo bodi hiyo inawasimamia na kuwalea kitaaluma hivyo hatua za kinidhamu ziweze kuchukuliwa kwa watu wote wa kada mbalimbali wanaohisika katika mradi huo.
Hata hivyo mkutano huo umeenda sambamba na kauli mbiu isemayo “fursa na changamoto katika kutekeleza ukuaji endelevu wa uchumi na maendeleo ya jamii”.