Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu, kazi ,vijana, ajira na watu wenye ulemavu,Patrobas Katambi akiongea katika kongamano la wanawake wenye ulemavu jijini linaloendelea mkoani Arusha
…………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu, kazi ,vijana, ajira na watu wenye ulemavu,Patrobas Katambi amesema kuwa serikali ipo katika hatua ya kufanya mabadiliko ya sera ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2004 kutokana na kupitwa na wakati ili kuweza kuweka sera zinazoendana na hali ya sasa katika kutatua changamoto zinazowakabili pamoja na kusimamia vizuri masuala yanayowahusu walemavu.
Katambi ameyasema hayo wakati akizingumza katika kongamano la wanawake wenye ulemavu jijini Arusha ambapo alisema kuwa alisema sera hiyo imepitwa na wakati kwani haiendani na hali ya sasa hivyo wapo katika mchakato wa mabadiliko ya sera ya watu wenye ulemavu.
“Tupo katika hatua ya kufanya mabadiliko ya sera ya watu wenye ulemavu kwani fedha zipo na watu wanakaa vikao hivyo wakati wa ushirikishwaji ni sasa ili kuingiza mambo yanahusu nyakati za kisasa,”alisema Katambi.
Aidha aliongeza kuwa watu wenye ulemavu kwa miaka 10 hadi 20 wanatekeleza sera iliyopita na wakati hivyo ipo haja ya kufanya mabadiliko kwani mambo ya zamani hayawezi kuwa ya kisasa na niwakati wa serikali kufanya kile kinachohusu kundi hilo.
“Serikali inafanya hivi kwasababu tunatambua watu wenye ulemavu mbali nakuona kuwa hawawezi kufanya chochote mimi nathibitisha sio kweli kwani wanauwezo wa kufanya kazi,elimu pamoja na vitu vingine,”alisema Katambi.
Alisema lazima watambue hutoaji wa haki kwa watu wenye ulemavu sio hisani bali ni lazima kutokana na wao ni binadamu kama wengine hivyo kila mmoja anaowajibu wa kuzitekeleza na kuzisimamia mujibu wa katiba wa nchi.
Naye Meneja wa mradi uongozi wa wanawake na haki za kiuchumi,Erasmina Massawe alisema wanawake wamekuwa wakibeba mzigo mkubwa wa kazi za nyumbani mara tatu zaidi ya mwanaume hali hiyo imepelekea kimweka mwanamke kuwa na uwezo mdogo kiuchumi na kijamii.
“Kwa Tanzania idadi ya watu wenye ulemavu inakadiliwa ni milioni 2.2 na kati yao asilimia 57.3 ni wanawake 42.7 ni wanaume ambapo wanawake wenye uleemavu wanabaguliwa zaidi kwa sababu ya ulemavu wao,”alisema Meneja huyo.