Uncategorized

ELIMU ZAIDI INAHITAJIKA KUMALIZA UKATILI WA KIJINSIA,MIMBA ZISIZOTARAJIWA

Written by mzalendoeditor
Na Mwandishi Wetu-DODOMA
Matukio ya ukatili wa kijinsia yanaongezeka kwa wasichana na kupelekea kupata ujauzito kwa kubakwa na ndugu wa karibu katika familia kama baba, mjomba au kaka.
Hayo yamebainishwa na Saida Husein kutoka jukwaa la Utu Mwanamke katika semina ya wanahabari  kupinga ukatili katika siku 16 inayoendelea jijini Dodoma.
”Sheria ya Tanzania hairuhusu utoaji mimba isipokuwa tu kama ujauzito utahatarisha maisha ya mwanamke, hicho ni chanzo cha wanawake kupoteza ndoto zao kutokana na mimba zitokanazo na kufanyiwa ukatilii wa kingono”
Kutokana na hilo Saida  amesema inapaswa elimu  kutolewa  kwa jamii ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ili kuepuka na mimba zisizotarajiwa

About the author

mzalendoeditor