Featured Kitaifa

WANAFUNZI WATAHADHARISHWA MATUMIZI MITANDAO YA KIJAMII, WATAKIWA KUTOTOA ‘PASSWORD’ ZA SIMU ZAO NA WAPENZI WAO

Written by mzalendoeditor

   

WANAFUNZI wa vyuo vikuu na vyuo vya kati wametakiwa kuwa makini katika kutunza taarifa zao binafsi na kuwa na matumizi salama ya mtandao.

Rai hiyo imetolewa na Mtaalamu wa makosa ya mtandano na uchunguzi wa makosa ya kidigitali, Yusuph Kileo wakati wa kutoa mada katika Chuo cha Uhasibu Arusha.

Hatua hiyo ni mwendelezo wa mpango wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa kutoa elimu kuhusu sheria mpya ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi na Sheria ya makosa ya Mtandao.

Alisema ni vyema wanafunzi hao wakawa na utaritibu wa kutiunza nywila (neno la siri) na kuchana na tabia na kushirikiana na watu wengine kutokana na ukaribu wao na watu hao.

“Tumetoa mafunzo maalum kwa wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha, kuhusu jinsi ya kulinda taarifa zao zinazopatikana kwenye vyombo vyao ya kieletroniki ikiwa ni simu au laptop kwani wasipofanya hivyo watajikuta taarifa zao binafasi zinajikuta katika maeneo ambayo si salama, maeneo ambayo hawakutarajia na kwa wahalifu wa mtandao.”

“Wanachopaswa kufanya ni kutoshirikisha watu wengine neno la siri na kuweka kuwa madhubuti ili isiwe rahisi kwa mtu ambaye si muhisika kuwenza kuzipata kirahisi

“Pia kuna wengine wanashirikisha neno la siri na mpenzi wake, mzazi au mtu mwingine anayemwamini na ikitokea kutokuelewana basi taarifa zao binafsi unazikuta mtandaoni wakati wewe mwenyewe uliruhusu kutoa neno la siri kwa mtu mwingine.”

Kileo pia alitoa tahadhari kwa wanafunzi hao kuwa makini na watu wanaoomba taarifa za neno la siri kwa njia ya barua pepe(emails) au kwa ujumbe wa simu ya mkononi.

“Hakuna kampuni ya simu au benki inaweza kukuuliza neno la siri kupitia njia yoyote kama ni email, au njia nyingine yoyote ile akatokea mtu kukuliiza usitoea iwe kwa email au simu usitoe.”

Naye Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Innocent Mungi alisema mafunzo hayo ni mwendelezo wa mkakati wa wizara wa kutoa elimu ya usalama wa mtandano kwa makundi mbalimbali katika jamii.

“Tanzania inaelekea kwenye uchumi wa kidigitali, hivyo tumeona ni muhimu wale wanaohusika na tasinia hii wapate elimu hii muhimu ya usalama wa matandao.”

“Tunawapa tahadhari kwa wale wanaokuja kufanya hizo kazi, lazima wajue hatari ambazo ziko katika mtandao ili kuweza kusaidia Serikali, taasisi na wananchi kwa ujumla umuhimu wa mausala ya ulinzi wa taarifa zao binafsi, kwani taarifa wanazoziweka kwenye mtandao wanaweza jikuta wanakosa ajira na kuaminika wakati taarifa ulizitoa kwa idhini yao bila kujaua madhara yake.”

Kwa upande wa Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Usalama Mtandao kutoka Wizara hiyo, Mhandisi Stephen Wangwe alisema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya watu wakimwemo wanasiasa na wasanii kudhalilishana kwenye mitandao ya jamii kwa kutumia taarifa binafsi za watu au kuingilia kaunti za mitandao ya jamii na kuwa njia pekee ni kuondokana na hali hiyo ni kuwa na matumizi salama ya teknolojia.

Alisema pia kumekuwepo na changamoto ya utapeli wa kutuma ujumbe mfupi na kuwasisitiza kuwa Serikali imekuja na mfumo wa kupambana na watu hao.

“Ukipata ujumbe wa matapeli hakikisha unatoa taarifa kupitia namba 15040, na sisi tunachambua na tunaifungia line ya simu, kifaa alichotumia na namna ya NIDA aliyotumia kusajili, tunaamni kwa nnjia hii tutapunguza matapeli.”

Wangwe aliwataka wanafunzi hao kutumia mitandao ya kijamii kichanya kutokana na kuwa na fursa nyingi kama vile kuwa jukwaa la biashara na kuongeza wateja.

“ Msijaribu kutumia mitandao ya jamii kuweka picha za siri, au video au chochote ambacho kinaweza kuharibu sifa na fursa ya kuwa na heshima katika jamii kwani kukiweka picha haifutiki hata kama wewe utaona umezifuta.”

Pia amehimiza haja ya jamii kutoa taarifa Polisi pindi unapotokea uhalifu wa kimtandano ili kuruhusu vyombo vya dola kufanyia kazi uhalifu huo na kuwa na takwimu za matukio kwani lengo ni kuhakikisha wananchi wanakuwa salama.

Kwa upande wake mwanafunzi wa chuo hicho mwaka wa tatu, Nembres Emmanue aliishukuru wizara kwa mafunzo hayo ambayo alisema yamewapa mwanga wa kukabiliana na changamoto za tekinolojia.

Mwanafunzi Derick Francis anayesoma Kompyuta Sayansi mwaka watatu, alisema kutokana na umuhimu wa mafunzo hayo ni vyema yakawafikia watu wengi kwani waathirika pia ni watu wasiosoma masomo hayo na kuwasihi vijana wenzake kuwa na matumizi sahihi ya tekinolojia ya habari.

About the author

mzalendoeditor