Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa wa Heshima ikiwa ni Shahada ya Udaktari wa Juu katika Humanitia na Sayansi Jamii na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa Cheti mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa wa Heshima ikiwa ni Shahada ya Udaktari wa Juu katika Humanitia na Sayansi Jamii na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda akizungumza katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar  akizungumza katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof.William Anangisye akizungumza katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

…………………………..

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametoa wito kwa Vyuo Vikuu kupitia mitaala yake ili ijikite katika kutoa elimu ambayo inakidhi mahitaji ya jamii. 

Rais Samia ametoa wito huo leo mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Doctor of Letters – Honoris Causa) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Mahafali ya 52 Duru ya Tano ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City.

Aidha, Rais Samia amesema mitaala hiyo itawezesha kutoa elimu ambayo inalenga kutoa wahitimu wenye weledi, wanaoajirika na wajasiriamali.

Rais Samia amesema pamoja na kuwa na uhuru wa kitaaluma, vyuo vikuu vina wajibu wa kutoa mchango wake katika kuleta maendeleo, kutoa elimu stahiki, kufanya tafiti na kutoa maoni ili kulikuza na kuliimarisha taifa letu.

Rais Samia pia amesema elimu inayotolewa na taasisi za elimu ya juu inapaswa kuwawezesha wahitimu kujiajiri, kuajiriwa, kuwa wajasiriamali na kuwa tayari kuchangia maendeleo ya taifa letu.

Vile vile, Rais Samia amevitaka vyuo vikuu kuwa na mikakati na malengo yanayolenga kufikia juu zaidi katika mzani wa kimataifa. 

Hali kadhalika, Rais Samia amesema Serikali inafuatilia na kutoa mchango kwa kuweka Sera na mikakati ambayo inajumuisha kuendelea kuongeza bajeti ya elimu.

Previous articleWAZIRI MKUU AHIMIZA ELIMU YA BIMA AFRIKA
Next articleCCM:SHAHADA YA UDAKTARI KWA RAIS SAMIA NI MATOKEO YA KAZI KUBWA,NZURI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here