Featured Michezo

SIMBA YANG’ARA UGENINI PHIRI AMJIBU MAYELE

Written by mzalendoeditor

SIMBA imetakata ugenini baada ya kuichapa mabao 3-1  timu ya Polisi Tanzania mchezo wa Ligi Kuu NBC Tanzania bara uliopigwa uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Mabao ya Simba yamefungwa kupitia kwa John Bocco pamoja na Moses Phiri aliyefunga mabao mawili na kufikisha mabao nane na kuendelea kufukuzia kinara wa mabao Fiston Mayele akiwa na mabao 10.

Bao  pekee la Polisi Tanzania limefungwa na Zuberi Khamisi dakika za  lala salama.

Kwa ushindi huo Simba wamefikisha Pointi 31 na kupanda hadi nafasi ya pili wakiwa wamecheza mechi 14 huku Yanga wakiendelea kuongoza wakiwa na Pointi 32 wakiwa wamecheza mechi 12.

About the author

mzalendoeditor