Featured Kimataifa

WAZIRI KIJAJI AZIHIMIZA NCHI ZA AFRIKA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI KATIKA KUFANYA BIASHARA

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amezihamasisha nchi za Afrika kutumia lugha ya kiswahili ili kuondoa changamoto ya lugha katika kufanya biashara ili kuleta maendeleo ya viwanda.

Aidha Waziri Kijaji amewataka wafanyabiashara wa Tanzania kuzalisha bidhaa zenye viwango vya kimataifa ili kikidhi usindani wanapotumia fursa za soko la Eneo Huru la Biashara Afrika ( AfCFTA)

Waziri Kijaji ameyasema hayo Novemba 23, 2022 wakati akishiriki katika Mkutano ngazi ya Baraza la Utendaji la Mawaziri katika Mkutano wa 17 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Maendeleo ya Viwanda Barani Afrika uliofanyika Novemba 20-25, 2022 Niamey, Niger.

Aidha, Waziri Kijaji atamwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano ngazi ya Wakuu wa Nchi na Serikali unatarajiwa kufanyika tarehe 25 Novemba, 2022.

About the author

mzalendoeditor