Featured Kitaifa

TRA MKOA WA MOROGORO YADHIBITI UPOTEVU WA MAPATO.

Written by mzalendoeditor
NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO.
MAMLAKA  ya Mapato Tanzania  (TRA) mkoa wa Morogoro, imesema kuwa imefanikiwa kudhibiti upotevu wa mapato na ukwepaji kodi kwa kufanya ukaguzi yakinifu na kudhibiti magendo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu na kuhimiza ulipaji kodi wa hiari kwa wafanyabiashara.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya shukrani kwa mlipakodi meneja wa TRA Mkoa wa Morogora Godwin Balongo alisema kuwa sababu ya mafanikio ni kuendelea kuwatambua na kuwasajili walipa kodi wapya,ushirikiano mzuri na wapamoja baina ya uongozi na wafanyakazi wa TRA .
“Kutumia vizuri mbinu tulizojiwekea ili kufanikisha malengo ikiwa ni pamoja na hizi kwa pamoja ndizo sababu zilizotufanya tupate mafanikio makubwa kwa mwaka huu wa fedha 2022 “alisema.
Aidha Balongo alieeleza kuwa dhima ya maadhimisho ya mlipa kodi ni kutambua mchango na ushirikiano uliopo baina ya TRA na wadau wake.
Alisema TRA kupitia maadhisho haya imekuwa ikiwaweka pamoja wadau wake kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii,burudani,kupata mrejesho wa wateja wao kutoa tuzo mbalimbali kwa wadai ambapo maadhimisho hayo yamebeba ujumbe, “ASANTE KWA KULIPA KODI KWA USTAWI WA JAMII NA MAENDELEO YA NCHI YETU.KAZI IENDELEE”
“Kupitia ujumbe huu tunaamini wananchi wanathamini matunda ya kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ambayo tumekuw tukiyashuhudia kwa serikali kuimarisha huduma za kijamii kama vile elimu, Afya na michezo, ujenzi wa miundombinu pamoja na huduma ya ulinzi na usalama.”alisema.
Balongo aliseleza kuwa katika kusherekea wiki ya mlipa kodi wametekeleza majukumu yafuatayo kufanya vikao na wadau wa mamlaka meneja wa Bank na washauri wa kodi, kutoa elimu ya kodi mashuleni.
” Tumetoa elimu katika shule ya sendari Yespa pia elimu ya mlipa kodi kwa kundi la nyumba za kulala wageni pamoja na hoteli,kutoa michango ya hisani michango kwenye kituo cha Mgolole kilichopo Bigwa ambacho kinahudumia watoto  yatima na kituo cha RAYA islamic centre kilichopo Mvomero.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhisho hayo ambapo alitoa wito wa kupanua wigo wa mapato ya serikali kwa kila mwananchi kutimiza wajibu wake na kuzingatia kutumia mashine za EFD, wafanyabiashara wote kutoa risiti na wanunuzi kudai risiti sahihi kwa wakati wote ,Kujisajili na kupata namba ya vitambulisho kwa Mlipa kodi (TINI) pamoja na leseni ya biashara.
“Pia wafanyabiashara wanapaswa kusajiliwa kwenye kodi ya ongezeko la Thamani VAT wafanyr hivyo kwa kuomba kusajiliwa kwenye mfumo huo ikiwa ni pamoja na kusajili pikipiki katika mfumo mpya wa namba zinazofuatana na za magari.”alisema.
“Taarifa ya usimamizi wa mapato iliyotolewa inatia moyo lakini bado inatupa picha kwamba kujitahidi kuziba pengo kuziba pengo liloanishwa kwa mwaka ujao”alisema.
Naye mwenyekiti wa   Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture ( TCCIA ) mkoa wa Morogoro Mwafhini Mnyanzo aliipongeza mamlaka hiyo kwa kutoa tunzo kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa vinara kwa kuwa walipaji kodi hodari huku akiomba kuboleshwaji wa vipengele kwa walipakodi hususani kwa wafanyabiashara wa holelini.
Aidha Mnyanzo ambaye alikuwa akiwawakilisha wafanyabiashara  aliomba mamlaka hiyo kufanya hafya hiyo kila mwaka kwani kufanya hivyo kutahamasisha ongezeko la ulipwaji kodi.

About the author

mzalendoeditor